WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo, akikagua Soko la Ndugai ziara aliyofanya leo March 2,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo, akitoa maelezo alipofanya ziara katika Soko la Ndugai leo March 2,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo,akimsikiliza Mwenyekiti wa Mawakala Bw.Zacharia Mmari mara baada ya kufanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika Kituo cha Mabasi Nane Nane leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Muonekano wa Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo,akiendelea na ziara ya kukagua utendaji kazi katika Bustani ya Chinangali Park ziara aliyoifanya leo March 2,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru,alipotembelea na kujionea maendeleo ya Chinangali Park ziara aliyoifanya leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Muonekano wa sehemu zilizopo Chinangali Park iliyopo jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo,akitoa maelezo katika kituo cha Malori kilichopo Nala jijini Dodoma mara baada ya kufanya ziara ya kukagua kituo hicho leo March 2,2021.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akimsikiliza Dereva Mwanamke Bi.Modersta Syprian anayeendesha malori kwenda nchini Sudan katika kituo cha Malori kilichopo Nala jijini Dodoma mara baada ya kufanya ziara ya kukagua kituo hicho leo March 2,2021.
Malori yakiwa yamepaki kwa ajili ya safari yaliyopo katika kituo cha Malori kilichopo Nala jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo, leo amekagua utendaji wa miradi ya kimkakati ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kutoa maagizo kadhaa ikiwamo ya kubuni mbinu mbalimbali ili kuongeza mzunguko wa biashara kwenye maeneo hayo.
Miradi hiyo ni pamoja na Kituo cha mabasi cha nanenane, Soko la Job Ndugai, Bustani ya kupumzikia ya Chinangali park na maegesho ya malori iliyopo Nala.
Ujenzi wa miradi huo umegharimu zaidi ya Sh.Bilioni 89 kupitia mradi wa Mradi wa Uendelezaji Miji Mkakati(TSCP) unaosimamia na TAMISEMI.
Akiwa katika soko la Ndugai, Waziri Jafo ameonesha kutofurahishwa na utendaji kazi wa soko hilo kutokana na kutokuwepo mzunguko wa biashara.
Amesema serikali imejenga miundombinu hiyo ya mabilioni ya fedha kwa ajili ya wananchi lakini ufanisi wake bado hauonekani na kutaka kuwekwa mbinu mbalimbali za kuongeza mwamko na mzunguko wa biashara kwenye miradi hiyo.
“Yaani kutokana hapa hadi mjini kati ni umbali wa kilomita nane, inashangaza kuona mradi huu ambao umekamilika kwa muda mrefu wa soko lakini mwamko wa biashara hakuna na maeneo mengine bado hakuna wafanyabiashara, hii kwa kweli haijaniridhisha,”amesema.
Ameagiza Jiji hilo kuhakikisha malori yote ya mizigo ya masokoni kushusha kwenye soko hilo ili kuongeza mwamko wa biashara.
“Nataka soko hili liwe ‘busy’, haiwezekani muwekewe miradi mikubwa ya gharama kubwa halafu haina watu, sijaridhishwa kabisa na hili soko hakuna kinachofanyika,”amesema.
Katika kituo cha mabasi, Waziri Jafo ameagiza Halmashauri hiyo kushughulikia kero zilizopo kwenye kituo hicho ili kifanye kazi kwa ufanisi.
Pia ameagiza kuwekwe mashine za kukusanya mapato kwa kila geti ili kurahisisha utendaji kazi na ukusanyaji mapato kutokana na kwasasa watu wanaoingia kwenye kituo hicho kutumia geti moja na kuwa kikwazo kwao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru, ameahidi kushughulikia maelekezo ya Waziri huku akisema katika soko hilo ndani ya wiki mbili kunatarajia kuwekwa gulio na shughuli zingine za kiuchumi jambo ambalo litaongeza mzunguko wa biashara kwenye eneo hilo.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Binilith Mahenge amesema uongozi wa Mkoa utahakikisha shughuli za kibiashara kwenye maeneo hayo zinachangamka na hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuleta ufanisi.
Katika mradi wa maegesho na bustani ya Chinangali, Waziri Jafo ameoneshwa kufurahishwa na utendaji kazi wako huku akiagiza Jiji hilo kuangalia uwezekano wa kumuongezea mtu anayeendesha bustani hiyo muda wa miaka mitatu badala ya mmoja.