Waziri wa Katiba na sheria Dkt Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki ya mtoto hapa nchini mpango unaolenga kuboresha upatikanaji wa haki ya mtoto, uzinduzi uliofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na sheria Dkt Mwigulu Nchemba,akisitiza jambao wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki ya mtoto hapa nchini mpango unaolenga kuboresha upatikanaji wa haki ya mtoto, uzinduzi uliofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na sheria Dkt Mwigulu Nchemba akizindua mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki ya mtoto hapa nchini mpango unaolenga kuboresha upatikanaji wa haki ya mtoto, uzinduzi uliofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki ya mtoto hapa nchini mpango unaolenga kuboresha upatikanaji wa haki ya mtoto, uzinduzi uliofanyika loe March 2,2021 jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Unicef hapa nchini Bi Shelini Baragua akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki ya mtoto hapa nchini mpango unaolenga kuboresha upatikanaji wa haki ya mtoto, uzinduzi uliofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Mwigulu Nchemba wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wawakilishi kutoka Wizara mbalimbali zinazotekeleza mpango mkakati endelevu ya haki mtoto hapa nchini wakiwa wameshika mpango mkakati huo baada ya kuzinduliwa leo March 2, 2021 Jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba amezindua mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki mtoto nchini ya mwaka 2020 hadi 2025 unaolenga kuboresha mapambano dhidi ya ukatili kwa Watoto huku akimuagiza Katibu Mkuu Wizara hiyo mpango huo kutafsiliwa kwa lugha ya Kiswahili.
Akizundua mpango huo leo March 2, 2021 Jijini Dodoma Dkt Nchemba amesema uzinduzi wa mpango huo ni nia ya serikali katika kupambana na ukatili kwa Watoto na kuimarisha haki ya mtoto na kutaka mpango huo utafsiliwe kwa lugha adhimu ya Kiswahili ili kila mmoja aweze kuuelewa mpango huo.
“Tulikuwa na mpango wa kwanza uliotekelezwa kuanzia mwaka 2012 hadi 2017 kuna mazuri yamefanyika lakini tumekuja na mpango huu ambao umeboreshwa zaidi na hii ni nia serikali kuhakikisha inalinda haki ya mtoto,
“Katibu mkuu nikuagize mpango huu utafsiliwe kwa lugha ya Kiswahili sote tunajua hii ni lugha ya ukombozi kwa nchi yetu hivyo ni vema mpango huo utafsiliwe kwa lugha ambayo kila mmoja wetu ataielewa wakati ya kuitekeleza” amesema Dkt Nchemba.
Amesema mpango huo umelenga Zaidi katika kuongeza uelewa wa haki ya mtoto katika jamii kwa Watoto na wadau mbalimbali, kuimarisha mfumo wa utoaji haki kwa mtoto, kuimarisha mfumo wa ulinzi na usalama wa mtoto, kuboresha sera na sheria, kuimarisha uratibu na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mpango mkakati huu.
Amongeza kuwa “Wizara ya katiba na sheria kwa kushirikiana na jukwaa la haki mtoto itaendelea kuratibu na kufuatilia mwenendo na utekelezaji wa mkakati huu kwa kushirikana na Wizara nyingine zinazotekeleza mpango huu” amesema.
Ametoa wito kwa wadau na jamii mbalimbali kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kutekeleza mpango mkakati huo ili Watoto waweze kulindwa na kufurahia upatikanaji wa haki kwa wakati kwa kuwa haki ya mtoto ni mtambuka.
Aidha amezitaka wizara na taasisi zote zinazotekeleza mpango huo kutoa tathmini ya taarifa kwa kipindi Flani ili kwa Pamoja kuzitambua changamoto zinazowakumba na kushirikishana kisha kuzitatua ili haki ya mtoto iweze kulindwa.
Waziri Dkt Nchemba amezitaka taasisi, mashirika, wadau na jamii kwa ujumla wakati wa kutekeleza mpango huo kuangalia upande wa pili kwa kumuangalia mtoto huyo kwa Maisha yake ya baadaye na badala yake wajue kutofautisha kuvunja haki ya mtoto na maandalizi ya mtoto kwa Maisha yake ya baadaye.
“Mtoto ukimuandaa katika njia flani hata iacha hata akiwa mzee maandiko ya Mungu katika vitabu yanasema hivyo, sasa hivi mchaka mchaka mpaka kwa aliyekosea, kuandaa bustani imekuwa mpaka adhabu wakati ni wajibu kuwajenga vijana wetu Maisha ya kujitegemea tangu wakiwa wadogo” amesema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome, amesema katika kulinda haki ya mtoto Wizara iliandaa na kuratibu na kuutekeleza mpango huo wa pili ambapo wamefanya marekebisho mbalimbali ya sheria yote ni katika kulinda hali ya mtoto.
Jitihada nyingine ametaja kuwa ni kuongeza makahama zinazosikiliza haki za Watoto hadi kufikia mahakama 130 na kuwapa mafunzo maafisa 638 wa mahakama waliojengewa uwezo wa kusikiliza mashauri yanayohusu kesi za ukatili dhidi ya Watoto, na mawakili wa serikali na mawakili wa kujitegemea walijengewa uwezo wa kuendesha kesi kama hizo.
Amesema kesi mbalimbali za ukatili dhidi ya Watoto 63,023 zimesikilizwa na kuwapa haki sawa hata watoto wanaotoka katika kaya maskini ambapo walikuwa hawana uwezo wa kuwa na wakili waliweza kusaidiwa ili kuweza kupata haki yao.
Nae Mwakilishi Mkazi wa UNICEF hapa nchini Bi. Shalini Baragua ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kupambana kuhakikisha haki ya mtoto inalindwa katika ngazi zote mijini na vijijini.
Amesema ulinzi wa mtoto ni suala mtambuka hivyo ni wajibu wa kila mwanajamii kuhakikisha anakuwa mlinzi wa Watoto ili kujenga kizazi imara kwa miaka ijayo na kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.