NAIBU waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Injinia Adrea Kundo wa kushoto akifafanua jambo na kuzungumza na baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na watumishi pamoja na makampuni mbali mbali ya simu akiwemo mkuuu wa TCRA ili kuweza kupanga mikakati ya kuboresha sekta ya mawasiliano na kuondoa changamoto zilizopo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza wakati wa ziara hiyo ya Naibu waziri wa mawasialino ambaye alifanya ziara yake ya kikazi katika baaadhi ya maeneo yaliyopo katika Jimbo la Chalinze kwa ajili ya kujionea shughuli mbali mbali mabazo zinafanywa na makampuni ya simu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze iliyopo Wilayani Bagamoyo akitoa neno la shukrani wakati wa ziara hiyo ya kikazi ambayo imefanywa na Naibu Waziri wa mawasialino teknolojia ya habari ili kuweza kuzungumza na watumishi pamoja na shushuli zinazofanywa na makampuni ya simu.
NAIBU waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Injinia Adrea Kundo aliyevalia suti nyeusi akiwa amenyoosha mkono kwa ajili ya kuwapongeza viongozi wa halmashauri ya Chalinze kwa juhudi zao za kuweza kukamilisha ujenzi wa jingo jipya la halmashauri hiyo.
MkurugenZI Mtendaji wa Halmashauri ya Chaliznze Ramadhani Posi akitoa taarifa fupi ya masuala ya mawasaliano katika maeneo mbali mbali wakati wa ziara hiyo ambayo ilifanywa na Naibu Waziri wa mawasaliano tekonoliojia ya habari ili kujionea mwennendo wa kazi zinazofanyika.
Katibu Tawala wa wilaya ya Bagamoyo Kaslida Mgeni akimkaribisha Naibu Wazairi wa mawasiliano Teknolojia ya habari ambaye alifanya ziara yake ya kikazi katika halmashauri ya Chalinze pamoja na kutemnbelea baadhi ya maeneo ambayo yana changamoto ya mawasiliano.
Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano TCRA Kanda ya Mashariki Mhandisi Lawi Odiero akitoa maelekezo ya jinsi walivyojipanga kwa ajili ya kuboresha sekta ya mawasaliano katika maeneo mabali mbali katika ziara hiyo,(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
……………………………………………………………………….
NA VICTOR MASANGU, CHALINZE
NAIBU waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Injinia Adrea Kundo ameyaagiza makampuni mbali mbali ya simu kuhakikisha kwamba wanaweka mipango ya kufanya utafiti wa kina katika maeneo ambayo tayari yameweka uwekezaji wa kufunga mitambo yao ya minara ili kuweza kubaini uhitaji wa matumizi ya wananchi lengo ikiwa ni kuwaondolea adha na usumbufu wa ukosefu wa mawasiliano.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri ya Chalinze iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwai kwa ajili ya kuzungumza na watumishi pamoja na mamlaka zinazohusika na mawasiliano ili kuweza kujadili changamoto mbali mbali zilizopo na kuzifanyia kazi na kubioresha zaidi sekta ya mawasiliano.
Naibu Waziri huyo aliisema kwamba nia kubwa ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba inaborsha zaidi sekta ya mawasiliano katika maeneo mbali mbali hapa nchini hivyo ni vema wadau wa masuala hayo wanapaswa kuweka mikakati yao madhubuti ambayo itasaidia kuboresha mitambo yao ambayo wanaifunga ikiwemo kwenda kuiangalia na kuifanyia ukarabati mara kwa mara ili iweze kufanya kazi vizuri kulingana na mahitaji ya wananchi.
“Hapa kitu kikubwa napenda kuagiza kwamba makampuni haya ya simu inatakiwa sasa kuhakikisha wanafanya uwekezaji waao ambao unatija na kuwafikia wananchi katika maeneo husika lakii kikubwa zaidi ni kufanya utafiti wa maeneo husika hasa ili kutembelea minara amabayo inakuwa imefungwa kwa kipindi cha muda mrefu, lakini kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watuamiaji mitambo inashindwa kuwafikia na wananchi katika maeneo mengine kwa hivyo ili ninaliomba sana,”aliongeza Naubi Waziri huyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa juhudi mbali mbali amabzo inazifanya lakini amebainisha kwamba bado kuna baadhi ya vijiji katika jimbo lake kuna chanagamoto ya upatikanaji wa mawasilano ya mtandao hivyo wananchi wanapata shida sana katika suala zima la kuwasiliana.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Chalinze Ramadhani Posi waliongeza kuwa kumekuwepo na baadhi ya madhara yatokanayo na ukosefu wa mawasiliano hasa pindi kunapoibuka sakata la migogoro ya wakulima na wafugaji inakuwa ni chanagmto kupata taarifa kwa wakati na kuomba waongezewe ruzuku katika suala zima la mawasialino.
Kwa upande wake Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano TCRA Kanda ya Mashariki Mhandisi Lawi Odiero amebainisha kwamba lengo ambalo wamejiwekea ni kuhakikisha wanalinda na kuboresha sekta ya mawasiliano kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo mbali mbali ambayo imetolewa inafutwa bilaya kuvunjwa nia ikiwa ni kuhakikisha kwamba huduma na hiyo inaleta mabadiliko chanya.
“Kwa sasa mabadiliko katika sekta hii kwa kweli yameleta mabadiliko makubwa sana na kuweza kurahisiha na kubadili hata kasi ya maendeleo kutokana na kuendesha na kufanya shughui zetu za kuwasiliana hivyo kumesaidia kuongeza tija zaidi katika mambo mengine hata ya kubadilisha kasi ya maendeleo kwa wananchi wetu wa Tanzania,”alibainisha Mhandisi Odiero.
Kadhalika aliongeza kuwa kwa sasa TCRA kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa vyombo vya habari itawasaidia kwa hali na mali katika kuwapa miongozo mbali mbali ambayo itawasaidia kufungua redio mbali mbali za kijamiii ambazo zitakuwa zikitumika katika kuwafikishia ujumbe mbali mbali juu ya shughuli za kimaendeleo amabzo zinafanyika katika maeneo yao.