………………………………………………………………………………………….
Na Allawi Kaboyo – Biharamulo
Naibu Waziri wa maji Mhe. Mhandisi Mery Prisca Mahundi ameagiza kuanza mchakato wa kupeleka maji katika shule ya Sekondari Mububa iliyopo wilayani Biharamulo ili kuondoa kero hiyo kwa wanafunzi.
Naibu Waziri ameyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi wilayani Biharamulo leo February 28, mwaka huu iliyoanzia katika mradi wa maji Kabindi na baadae shule ya Sekondari Mububa
Akiwa katika mradi wa. Maji wa Kabindi, Naibu Waziri waipongeza wakala wa Maji Vijijini RUWASA Mkoani Kagera kwa Kasi waliyonayo katika kuhakikisha wanaondoka adha ya maji hasa kwa wilaya ya Biharamulo.
Ameongeza kuwa kutokana na jitihada ambazo RUWASA wilaya ya Biharamulo walizonazo, wizara itawaletea fedha kwaajili ya kupanua mtandao wa maji na kuanzisha miradi mipya kwenye maeneo ambayo bado Kuna kero ya maji.
“Niwaomgeze wananchi kwa kumchagu Mhe. Ezra Chiwelesa kuwa mbunge wenu, amekuwa akinisumbua kuhusu suala la maji na hapa nimekuja kufatia maswali take ya kutaka kumaliza kero ya maji Biharamulo,”
“RUWASA mnafanya vizuri niwapongeze Sana na kwanamna mnavyokwenda pesa tutaleta ili miradi mingi mliyonayo muweze kuimalizia.”
Akiwa katika shule ya Sekondari Mububa Naibu Waziri ameeleza kuanza mchakato wa kitaalamu ili kuweza kusogeza huduma ya maji shuleni hapo ambayo imekuwa changamoto ya muda mrefu na kupelekea wanafunzi kuhangaika.
Kwaupande wake mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Mhe. Mhandisi Ezra Chiwelesa, amesema kuwa wilaya hiyo imekuwa ikitengewa bajeti finyu na kupelekea Maeneo mengi kutopata huduma ya maji.
Mhe. Ezra ameongeza kuwa licha ya shule ya Sekondari Mububa kuwa na changoto ya umeme, changamoto mama ni maji ambayo imekuwa ikiwapelekea wanafunzi hao kutembea umbali mrefu na muda mwingine kukosa masomo.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa kata ya Kabindi wilayani Biharamulo mkoani Kagera wamesema katika kipindi ambacho miradi ya maji ilikuwa haijakarabatiwa walikuwa wanalazimika kunywa maji yasiyo safi na salama kutokana na kukosekana kwa maji ya bomba katika eneo hilo.
Hali hiyo imemsukuma naibu waziri wa maji Mery Priscar Mahundi kufika katika kata hiyo na kuzindua mradi wa maji uliogharimu kiasi cha shilingi milioni mia tatu ishirini na tano utakaoweza kuwahudumia vijiji vinne vyenye zaidi ya wananchi elfu kumi na nane(18,000).