Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Raslimali watu wa wizara ya viwanda na biashara Bi Veronica Nchango akizungumza wakati akifunga mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi wa Wizara hiyo yaliyofanyika katika Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma kuanzia Februari 23 hadi 25, 2021. Mafunzo yalilenga kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa Wizara hiyo ili kuleta tija mahala pa kazi.
Mkuu wa kitengo cha KAIZEN Tanzania ambaye ni afisa Biashara Mkuu Wizara hiyo Bi Jane Lyatuu akifafanua jambo kwa wajumbe wakati ya kuhitimisha mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara yaliyofanyika katika Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma kuanzia Februari 23 hadi 25, 2021. Mafunzo yaliyolenga kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa Wizara hiyo ili kuleta tija mahala za kazi.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda Bw. Gaitan Mrimi akitolea ufafanuzi jambo wakati ya kuhitimisha mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara yaliyofanyika katika Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma kuanzia Februari 23 hadi 25, 2021. Mafunzo yaliyolenga kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa Wizara hiyo ili kuleta tija mahala za kazi.
Mkufunzi wa KAIZEN Bw. Emanuel Zakayo akitoa majumuisho mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kutembelea viwanda wakati ya kuhitimisha mafunzo ya KAIZAN kwa watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara yaliyofanyika katika Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma kuanzia Februari 23 hadi 25, 2021. Mafunzo yaliyolenga kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa Wizara hiyo ili kuleta tija mahala za kazi
Mratibu wa mafunzo ya KAIZEN ambaye ni Mhandisi wa Wizara hiyo Eng. Kamala Gombe akifafanua jambo wakati ya kuhitimisha mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara yaliyofanyika katika Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma kuanzia Februari 23 hadi 25, 2021. Mafunzo yaliyolenga kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa Wizara hiyo ili kuleta tija mahala za kazi.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mafunzo ya KAIZEN wakiangalia bidhaa aina ya wine zinazotengenezwa na kiwanda cha Dane Holding wakati walipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mkulabi Mpunguzi Jijini Dodoma.
Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Dane Holding Limited Bw. Meshack Yotam kulia akitoa maelezo ya namna kiwanda hicho kinavyofanyakazi au moja ya njia katika uzalishaji wa wine kwa watumishi wa Wizara ya Viwanda waliohudhuria mafunzo ya KAIZEN walipotembelea kiwanda hicho kuona KAIZAN inavyotekelezwa mahala pa kazi.
Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Glory Farm kilichopo Nane nane Jijini Dodoma kinachojihusisha na uzalishaji wa mafuta ya alizeti Bw. Denis Kokino akionesha moja ya mtambo wa kusafisha mafuta ya alizeti kwa watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara waliohudhuria mafunzo ya KAIZEN walipotembelea kiwanda hicho kwa mafunzo.
Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Glory Farm kilichopo Nane nane Jijini Dodoma kinachojihusisha na uzalishaji wa mafuta ya alizeti Bw. Denis Kokino akitolea ufafanuzi moja ya jambo kwa watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara waliohudhuria mafunzo ya KAIZEN walipotembelea kiwanda hicho kwa mafunzo.
Afisa Tawala mwandamizi wa Wizara hiyo. Bw. Juma Mantatakala akionesha moja ya mtambo wa kusafisha mafuta ya alizeti akitaka kujua namna unavyofanya kazi, wakati watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara waliohudhuria mafunzo ya KAIZEN walipotembelea kiwanda cha kukamua na kusafisha mafuta cha Glory Farm kilichopo Nane nane Jijini Dodoma kwa mafunzo ya vitendo.
………………………………………………………………………………………….
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Raslimali watu wa wizara ya viwanda na biashara Bi Veronica Nchango amewasisitiza watumishi wa Wizara hiyo kuishi maisha kwa kufuata misingi ya Falsafa ya KAIZEN inayowahimiza kuzingatia udhibiti wa mazingira ya kazi na kuboresha usimamizi wa raslimali kama vile Mda Watu na Fedha ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano.
Bi Nchango ameyasema hayo alipokuwa akifunga mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi wa Wizara hiyo yaliyofanyika katika Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma kuanzia Februari 23 hadi 25, 2021. Pia Amewasisitiza watumishi hao kuzingatia ubunifu, ubora na tija ili kupunguza malalamiko, upotevu na gharama zisizokuwa za lazima katika utendaji kazi.
Amewahimiza watumishi hao kuwa chanzo cha mabadiliko katika utendaji wao na wawafundishe watumishi wenzao katika wizara nyingine pamoja na familia zao wakiwemo watoto wao ili wakue katika misingi ya kufanya kazi kwa ufanisi, tija na ubora nchini.
Aidha, Mkurugenzi huyo amewashauri wakufunzi wa Falsafa ya KAIZEN kuongeza S moja inayomaanisha “Sensitization” ili kuhamasisha watu zaidi kujifunza na kutekeleza falsafa hii katika kuongeza tija na ubora. “S” nyingine (5) tano zinazotumika kama njia za utekelezaji wa KAIZEN ni Sasambua (Sort), Seti (Seti), Safisha (Shine), Sanifisha (Standardize) na Shikilia (Sustain).
Ameshauri mafunzo hayo yaliyolenga kuongeza ufahamu kuhusu falsafa KAIZEN inayolenga kuongeza thamani endelevu ya tija na ubora viwandani yaingizwe kwenye mitaala ya shule na yafundishwe nchi nzima ili kuhimili kufikia matokeo bora, makubwa na kwa haraka na kuhimili ushindani.
Aidha, Mkurugenzi huyo aliwapongeza watumishi hao kwa kuhudhuria mafunzo hayo pamoja na kutembelea Viwanda vinavyotekeleza falsafa ya KAIZEN vilivyopo jijini Dodoma kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo. Viwanda hivyo ni Dane Holding Limited kinachotengeneza mvinyo na kiwanda cha “Groly Farm” kinachozalisha mafuta ya Alizeti.
Utekelezaji wa KAIZEN nchini unayofadhiliwa JICA unalenga kuongeza tija na ubora katika sekta ya viwanda na shughuli za maisha ya kila siku inaongozwa na misingi ambayo ipo katika ubunifu wa mawazo, maarifa na ushiriki wa kila mtu ndani ya taasisi, shirika au kampuni ili kuhimili ushindani.
KAIZEN ni neno la kijapani lenye maana ya badilika kwa ubora / uzuri linalohusu shughuli endelevu zinazofanyika ili kuboresha kazi mifumo michakato na nyanja yoyote ya kuendesha biashara. KAIZEN asili yake ni Japani lakini sasa inatekelezwa Duniani kote.