Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge ,akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakati wa kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo katika hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Gerald Kusaya,akizungumza kabla ya kuingia Makubaliano ya Mkataba na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo katika hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Utawala JKT ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi JKT Kanali Hassan Mabena,akitoa taarifa kabla ya kusainiwa mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo na Wizara ya Kilimo katika hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakitiliana sahihi ya Mkataba wa ushirikiano wa kuboresha sekta ya kilimo hafla iliyofanyika leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT, yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakibadilisha hati mara baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakionyesha hati ya mkataba mara baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) akimkabidhi zawadi ya saa ya ukutani Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya mara baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya akionyesha zawadi yake aliyokabidhiwa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),Meja Jenerali Charles Mbunge mara baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) akimkabidhi zawadi ya Note Book Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya mara baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) akimkabidhi Calendar Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya mara baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Gerald Kusaya,akipanda Mti mara baada ya kuingia Makubaliano ya Mkataba na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo katika hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Gerald Kusaya,akiumwangilia maji mti wake mara baada ya kuupanda mara kabla ya kuingia Makubaliano ya Mkataba na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo katika hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
……………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limeingia Makubaliano ya mkataba wa miaka mitano na Wizara ya Kilimo hapa nchini katika kuhakikisha wanakuza uchumi kupitia sekta ya kilimo.
Akizungumza kabla ya kusaini Mkataba huo leo Februari 26,2021 Mkoani Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Kusaya amesema kuwa amekuwa akifuatilia kazi za kilimo zinazofanywa na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) na kuamua kuingia nao mkataba kuinua sekta hiyo.
” Mara kwa mara nimekuwa nikifuatilia kazi za kilimo zinazofanywa na Jeshi letu tumeamua kuingia makubaliano haya kwa pamoja tuinue hii sekta” amesema Kusaya
Aidha Kusaya amesema kuwa kupitia makubaliano hayo kuna maeneo ambayo watapaswa kuwajibika ikiwa ni katika teknolojia bora ya uzalishaji mazao,kujenga uwezo wa kusambaza mbegu,utoaji huduma za umwagiliaji,utaftaji masoko ya mazao.
Kusaya amesema kuwa majukumu baada ya kusaini Mkataba huo watakuwa wakifanya utafiti pamoja katika mambo mbalimbali yanayohusu kilimo hapa nchi na upatikanaji wa mbegu bora.
Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge amebainisha kuwa Wizara ya Kilimo haitajutia makubaliano yaliyoingiwa kutokana na tija itakayopatikana.
“Makubaliano hayo yamekuja wakati muafaka kwani vijana wengi wa Tanzania wamekua wakijitolea kwenye mafunzo yetu ya JKT hivyo wakiwa ndani ya JKT watapatiwa mafunzo ya Kilimo ambapo tunahakika na wao wataenda kuitumia vizuri pindi watakapokuwa uraiani,”amesema Meja Jenerali Mbuge
Hata hivyo Meja Jenerali Mbuge ameongeza kuwa Jeshi ni chombo pekee ndani ya Taifa letu hivyo endapo likitumiwa vizuri litaleta manufaa makubwa katika Taifa.
Amesema kuwa JKT tayari limeshaanza shughuli za Kilimo kwa mazao ya kimkakati Katika maeneo mbalimbali ya hapa Nchini.
Aidha amemuomba Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Kusaya kutembelea skimu ya umwagiliaji iliyopo kikosi cha 837 KJ,Chita Mkoani Morogoro ambayo imelenga kuzalisha mara mbili kwa mwaka zao la mpunga.
Pia amebainisha baadhi ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo katika utekelezaji wa miradi yake ikiwemo wa skimu ya umwagiliaji ya Chita kuwa ni pamoja na ukosefu wa fedha katika kuziendeleza ziweze kuleta tija katika uzalishaji.
Awali, Kaimu Mkuu wa Utawala JKT ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi JKT Kanali Hassan Mabena amesema kuwa lengo la Mktaba huu ni kuhakikisha Taifa linajitosheleza kwa chakula na kulipunguzia Taifa mzigo.
“Jeshi la kujenga Taifa (JKT) limejiwekezea nguvu kubwa katika vikosi vyake kwani mazao yote ya kimkakati yanalimwa Katika vikosi hivyo,” Kanali Mabena
Kanali Mabena amebainisha changamoto wanazokumbana nazo katika Kilimo ni mabadiliko ya tabia nchi, na uhaba wa pembejeo za Kilimo.
Aidha Kanali Mabena ametaja vikwazo vingine ni upungufu wa wataalam wa kilimo ,mifugo na uvuvi na upungufu wa maabara za kupimia afya ya udongo na kutoa majibu kwa wakati