******************************************
Naibu Waziri wa Tamisemi David Silinde aagiza halmashauri ya Ndanda iliyopo mkoani Mtwara kujenga majengo mengine katika shule ya Msingi Mpowora baada kukuta madarasa mabovu kabisa ambayo yanaweza kuwaangukia wanafunzi mda wowote. Kauli hiyo ameitoa alipotembelea shule hiyo.
Kusoma katika mazingira mazuri na yenye majengo mazuri ni moja ya kishawishi kikubwa cha ufaulu wa wanafunzi katika mitihani yao lakini kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mpowora iliyopo Ndanda wilaya ya Masasi, mkoa wa Mtwara ni tofauti kwani kwa sasa wanafunzi katika shule hiyo wanatumia madarasa ambayo yamechoka sana huku yakiwa na nyufa ambazo zinawajengea hofu ya kusoma na kutimiza ndoto zao.
Japhet Anord na Shamira Bushiri ni wanafunzi wa shule hiyo wakiokba serikali yao kutenga fedha ya kuwajengea madarasa mapya baada ya madarasa kuwa hatarishi kwao ambayo hayana madirisha na kufanya mvua ikinyesha maji yao,jua likiwa kali lao huku mbao zikiwa zimeliwa na mchwa na kuwatengenezea hofu kwani mda wowote majengo hayo yanaweza waangukia.
Cecil Mwambe ambaye ni mbunge wa Ndanda na ni mwalimu mkuu wa shule hiyo wameiangukia serikali kuisaidia shule kwa kujengewa madarasa mapya kwani kwasasa hali ni mbaya zaidi huku walimu wa shule hiyo wakikosa vyoo vya kujisaidia na kuomba mkono wa serikali na wananchi wapo tayari kuchangia.
Kwa upande wa serikali kupitia kwa Naibu waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde ambaye alifika shuleni hapo kujionea mazingira wanayosomoa wanafunzi hao na kuahidi kuingiza fedha kiasi cha milioni 40 siku hiyo ambayo ni nje ya bajeti na kuwaahidi wanafunzi na walimu kuwa shule hiyo itaingizwa katika bajeti ya kuwajengea madarasa mengine mapya na kuwa yeye hajaridhika kabisa na mazingira ya wanafunzi wanaposomea.