Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binirith Mahenge akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dk.Suleiman Serera wakikagua ujenzi wa mradi wa maji kutoka bwawa la Mtera hadi kijiji cha Mtera ziara iliyofanyika leo Februari 25,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binirith Mahenge akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa maji kutoka bwawa la Mtera hadi kijiji cha Mtera ziara iliyofanyika leo Februari 25,2021.
Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge,akitoa maelezo kwa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka bwawa la Mtera hadi kijiji cha Mtera katika ziara iliyofanyika leo Februari 25,2021.
Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge akikagua mifereji iliyochimbwa kupitisha mabomba ya maji katika utekelezaji wa mradi wa maji kutoka bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Februari 25,2021.
Meneja RUWASA wa Wilaya ya Mpwapwa Eng. Cyprian Warioba (kushoto) akimueleza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge(Kulia) utekelezaji wa mradi huo wa maji kutoka bwawa la Mtera katika ziara iliyofanyika leo Februari 25,2021.
Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge,akifurahia jambo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ,Gilles Muroto mara baada ya kukagua na kujionea ujenzi wa mradi wa maji kutoka bwawa la Mtera hadi kijiji cha Mtera katika ziara iliyofanyika leo Februari 25,2021.
…………………………………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binirith Mahenge ameitaka Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka bwawa la Mtera hadi kijiji cha Mtera kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Dr. John Pombe Magufuli mwezi Septemba mwaka jana.
Agizo hilo amelitoa leo Februari 25,2021 wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo Dk.Mahenge amesema uwepo wa miundombinu na huduma za kijamii kama maji na umeme kutaongeza tija na kukuza uchumi wa mji wa Mtera ambao upo karibu na bwawa la Mtera ambalo linaweza kutumika kama kivutio cha utalii hivyo kuchelewa kwa mradi huo ni kurudisha nyuma juhudi za kuuinua maisha ya wakazi wa Mtera.
“RUWASA mmefanya kazi nzuri,lakini mnahitaji kuongeza kasi ili wananchi wa mji huu wapate huduma ya maji safi na salama.Pia uwepo wa maji utavutia uwekezaji mwingine ikiwemo vituo vya afya na biashara nyinginezo.”amesisitiza
Dk. Mahenge amewataka RUWASA kuhakikisha maji yanafika katika kituo cha afya cha kijiji cha Chipogolo ambacho ujenzi wake ulianza baada ya Rais Magufuli kutoa fedha mwaka jana ili kuboresha huduma za afya katika kijiji hicho ambacho nacho kipo katika barabara ya Dodoma kuelekea Iringa.
“Kituo kile kinaweza kuwa msaada mkubwa kwa hata kwa wasafiri wa barabara hii kubwa,hivyo maji lazima yafike pale mapema ili hata madaktari wasishindwe kuishi pale kisa ukosefu wa maji.” amesema Dkt.Mahenge.
Ikumbukwe wananchi wa kijiji hicho walimuomba Rais Magufuli huduma hiyo ya maji baridi kutoka Bwawa la Mtera alipokuwa anapita kuelekea mkoani Iringa akitokea mkoani Dodoma,Rais Magufuli aliagiza RUWASA kufikisha maji katika kijiji hicho.
Wananchi walalamika kutumia maji ya chumvi kwa muda mrefu ikiwa maji baridi yanapatikana karibu na kijiji na pindi walipoenda kuchota maji walivamiwa na mamba na viboko kutoka Bwawa hilo.
Kwa upande wake Meneja RUWASA wa Wilaya ya Mpwapwa Mhandis.Cyprian Warioba amesema mradi huo umekamilika kwa 95% tangu walipoanza utekelezaji wake tarehe 15 Disemba 2020 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili badala ya tarehe 15 Mwezi Machi kama ilivypangwa awali.
Naye Meneja wa RUWASA Mkoa wa Dodoma Dk. Godfrey Mbabaye amesema Mradi huo umegawanyika katika hatua mbili muhimu ambapo hatua ya kwanza ni ya muda mfupi ambayo inakaribia kukamilika na hatua ya muda mrefu ambayo itaanza hapo baadaye.