RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo (kushoto kwa Rais) akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Kitabu cha Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji wa Awamu ya Tatu 2017/2022 akikabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu kujitambulisha hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha akiongozana na Ujumbe wake na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA Bw. Makame Kh. Hassan (kushoto kwake) mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 25-2-2021.(Picha na Ikulu)