Kikundi cha Ngoma Asili cha Sarakasi wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo huo
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi mwenye kilemba cheupe akishiriki kucheza ngoma ya asilina wadau mbalimbali |
WAZIRI wa Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikagua baadhi bidhaa zilizoletwa na wadau mbalimbali
Kwaya ya Chuo cha Utumishi Singida wakitumbuiza wakati wa tukio hilo
Na John Mapepele, Singida
Waziri
kuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassimu Majaliwa
amezitaka Mamlaka zote za Mikoa kujipanga kikamilifu kutangaza fursa
za uwekezaji zinapatikana kwenye mikoa yao kwa kushirikiana Kituo cha
Taifa cha Uwezekezaji ili kuhakikisha kuwa fursa zote zilizoainishwa
kwenye miongozo ya uwekezaji zinapata wawekezaji makini ili kuongeza
mapato na ajira kwa wananchi
Akisoma hotuba ya Mheshimiwa
Waziri Mkuu kwenye tukio la uzinduzi wa Mwongozo wa Fursa za Uwekezaji
Mkoa wa Singida, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji Profesa Kitila
Mkumbo amesema kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano(5)
Serikali imedhamilia kuimarisha ustawi wa wananchi wake kwa kuzalisha
ajira milioni nane na kukuza uchumi wake kwa asilimia nane hivyo
uwekezaji makini unatakiwa ili kufanikisha azma hiyo.
Amesema
ili kuwapata wawekezaji makaini watendaji wote wa Serikali hawana budi
kutoa taarifa sahihi za fursa zinazopatikana katika maeneo yao na
utaratibu wote wa namna ya kuufuata ili kuweza kuwekeza.
“Ndugu
zangu ni muhimu sana tubadilike taarifa za uwekekezaji tunazozitoa
ziwe sahihi na ziwe zinafanana, ukienda kwa Mkuu wa Mkoa upate taarifa
sawa na ukichukua taarifa hiyo kwa Katibu Tawala wa Mkoa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hapo tutakuwa tumefanikiwa” amesisitiza
Profesa Mkumbo.
Amezitaka mamlaka hizo kutowakwamisha
wawekezaji kwa kuhakikisha maeneo ya uwekezaji yanapatikana mara moja
ili pindi Wawekezaji wanapofika wanapatiwa maeneo hayo na
wanahudumiwa kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto zozote
zinazojitokeza.
Amesema balozi namba moja anayeweza kuleta au
kutoleta wawekezazi katika nchi yoyote duniani ni Muwekezaji aliye
ndani ya nchi husika hivyo ni muhimu kuwapa huduma bora ili waweze
kutuletea wawekezaji wengi zaidi ambapo amesisitiza uwekezaji ufanywe
kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya Serikali ili nchi yetu
iweze kunufaika.
Amekemea tabia ya kupenda kutoa lawama baada
ya kuingia mikataba mibovu na wawekezaji na badala yake amewataka
watendaji kuwa makini katika mchakato mzima wa majadiliano na kufunga
mikataba hiyo na wawekezaji.
Aidha, ameitaka kila Mkoa kuangalia
kuangalia maeneo machache ya kipekee ili kufanya uwekezaji wenye tija
badala ya kwenda na maeneo mengi ambayo hayana tija.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais John Pombe
Magufuli kwa kubuni mikkakati kabambe ya uwekezaji ambayotayari katika
kipindi kifupi imeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii kwenye
nchi yetu.
Amesema Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa ambayo
ilikuwa ikionekana kama mikoa masikini lakini sasa umekuwa ni
miongoni mwa mikoa ambayo inaweza kuongoza kuleta mapato makubwa kwa
nchi kutokana na kuboreshwa kwa mazingira na fursa nyingi zilizopo.
Ametaja
baadhi ya fursa za uwekezaji zinazopatikana kuwa ni pamoja na madini,
kilimo cha Alizeti na Korosho, mafuta asilina na gesi pia elimu.