Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dk.Dorothy Gwajima akizungumza wakati akifungua kongamano na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) unaofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dk.Dorothy Gwajima akisisitiza jambo wakati akifungua kongamano na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) unaofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dk. John Jingu,akiwaeleza jambo washiriki wakati wa kongamano na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) unaofanyika jijini Dodoma
rais wa chama cha wataalamu wa maendeleo ya jamii Tanzania (CODEPATA) Bw. Wambura Sunday,akitoa taarifa kwa washiriki wakati wa ufunguzi wa kongamano na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) unaofanyika jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dk.Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) unaofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dk.Dorothy Gwajima,akikagua mabanda mara baada ya kufungua kongamano na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) unaofanyika jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima amemuagiza Katibu Mkuu Wizara hiyo idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu kufanya tathmini ya kina kwa Halmashauri zote kujiridhisha hali ya utekelezaji na utoaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotengwa kwa makundi maalumu kama inatengwa na kugawiwa kikamilifu kwa makundi hayo.
Dkt Gwajima ametoa maagizo hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa mwaka chama cha wataalamu wa maendeleo ya jamii hapa nchini CODEPATA waliokutana kujadili namna ya kuboresha taaluma hiyo, amesema kuna baadhi ya maeneo hawajafanya vizuri na elimu hiyo haijafika kikamilifu kwa wananchi.
“Nina simu yangu ya wananchi humo napokea taarifa nyingi sana wengine wanasema nisaidie kitu hiki lakini nawaambia mbona katika maeneo yenu kuna fulsa hii, wanasema waziri hatujui kabisa hicho kitu tuelekeze wapi tutaweza kupata” amesema Dkt Gwajima.
Ameongeza kuwa “Kuna baadhi ya maeneo elimu bado kabisa nataka ninyi maafisa maendeleo ya jamii mkaeneze taarifa hizi ninyi mko karibu sana na wananchi nendeni chini kabisa kila sehemu hata kanisani wapi fikeni wapate taarifa za uwepo wa mikopo hii iwasaidie
“Katibu upo hapa nenda kafanye tathmini katika halmashauri zote zimetekeleza kwa kiasi gani agizo hilo na halmashauri utakayokuta imetekeleza kwa kiwango cha chini niambie niende mimi mwenyewe nikaone shida ni nini haiwezekani wananchi wasinufaike na fedha hizi” amesema.
Amewataka maafisa maendeleo ya jamii kote nchini kuongeza kasi ya utoaji elimu ya mikopo hiyo inayotolewa na serikali na elimu bora ya namna ya kuimarisha vikundi hivyo na namna ya kujitegemea kwa vikundi hivyo ili waweze kunufaika na vikundi hivyo.
Amesema Serikali inatekeleza miradi mingi ya kimkakati ambayo yote itaweza kusaidia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka eneo moja kwenda eneo lingine amesema ni wajibu wa maafisa maendeleo ya jamii katika kutoa elimu kwa jamii itambue umuhimu wa miradi hiyo mikubwa na namna itakavyoweza kuwanufaisha wananchi hao.
Akizungumzia ukatili wa kijinsia amesema bado ni tatizo katika maeneo mengi hapa nchini ambapo ametaka kupatiwa taarifa za vitendo hivyo, ametaka maafisa maendeleo ya jamii kusimamia vitendo hivyo kupitia kamati za mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto “MTAKUWWA” katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hadi katika ngazi za chini kabisa.
Ameongeza kuwa “ wengine hawana kabisa hizi kamati za MTAKUWWA ninataka kupata taarifa rasmi ya kamati hizi katika ngazi zote nione je zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa” amesema.
Ameagiza maafisa maendeleo ya jamii kutenga siku maalumu kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wananchi yanayohusu ukatili wa kijinsia tu ili wananchi wapate mda mzuri wa kuripoti vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea ili vikomeshwe, huku akitaja mikoa ya Dar es saalamu, Arusha, Tanga, Manyara na Lindi ni miongoni mwa mikoa vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vipo juu.
Awali rais wa chama cha wataalamu wa maendeleo ya jamii nchini CODEPATA bw. Sunday Wambura amesema CODEPATA ilianzishwa mwaka 2017 na kuanza kufanyakazi rasmi mwaka 2019 baada ya kusajiliwa.
Amesema mpaka sasa chama hicho kimesajili wanachama 408 wakitoka katika sekta mbalimbali, huku akibainisha kuwa mkutano huo ni wa siku tatu ambapo watatumia katika kujadili mambo mbalimbali yanayohusu chama hicho katika kuboresha utendaji kazi wa taaluma hiyo hapa nchini.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto idara kuu ya maendeleo ya jamii Dkt John Jingu amesema mkutano huo ni wa nne tangu kuundwa kwa chama hicho na kubainisha kuwa chama hicho kimekuwa kikiimarika kadri siku zinavyokwenda, amesema chama hicho ni muhimu katika kusimamia taaluma ya wataalamu wa taaluma hiyo hapa nchini kwa kuwa maafisa maendeleo ya jamii wao wapo hadi ngazi za chini kabisa katika jamii.