Muonekano wa Jengo la Kliniki ya Mama na Mtoto lililopo Kata Kibirizi Kijiji Rwakaigwa ambalo Mhe. Rweikiza ametoa Milioni 8 liweze kumalizika ikiwa Ni ahadi yake aloitoa Mwaka Jana.
Jengo la Zahanati Kata Kagya ambalo Mhe. Rweikiza pia amehusika Kikubwa kupatikana kwa Wafadhili na Sasa lipo tayari kwa kutumika baada ya kulitembelea na kuridhika na Ujenzi wake
Daraja linalounganisha eneo la Ombueya na Kibirizi nalo limefikia hatua hii ambalo Mhe. Rweikiza alilisemea na kuahidi kuwa litatengenezwa na litaanza kupitika hivi karibuni.
Mhe. Rweikiza akikabidhi Shilingi Laki Mbili na Nusu Kama utekelezaji wa ahadi yake aloitoa ya kulipa Mshahara wa Mlinzi Kliniki pia laki Mbili na Nusu nyingine imelipwa kwa Mlinzi wa Zahanati Kibirizi
Mhe. Rweikiza akikabidhi Mipira miwili kuunga Mkono juhudi za Michezo Shule ya Sekondari Kibirizi, ambapo Mipira Kama hiyo wamepewa pia Shule ya Sekondari Tunamkumbuka.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tunamkumbuka Wakifurahia na Mbunge wao Mara baada ya kuwapa Shilingi laki Mbili na Mipira miwili
*********************************************
Dkt Jasson Samson Rweikiza ameanza Ziara yake ya Kushukuru na kukamilisha ahadi alizozitoa kipindi cha Kampeini, huku akibaini Miradi mipya na changamoto mpya katika Jimbo la Bukoba Vijijini kwa kutembelea Kata mbalimbali za Jimbo lake ambapo ameanza na Kata za Butelankuzi, Kibirizi na Kagya.
Mhe. Rweikiza amefika Kata Butelankuzi na kukutana na Walimu na Wanafunzi wa Shule za Sekondari Tunamkumbuka, pamoja na Shule ya Sekondari Kibirizi na ya Kata Kibirizi ambapo katika Shule ameshukuru kwa namna walivyompigia Kura kwa Wingi na Kuwaachia Pesa Shilingi laki Mbili kila Shule za Sukari ya Uji pamoja na Mipira miwili miwili ya Michezo
Aidha kwa Upande Mwingine Mhe. Rweikiza akiwa Kata Kibirizi ametembelea Kliniki ya Mama na Mtoto ya Rwakaigwa inayojengwa katika Kijiji Ombueya na kujionea jitihada zilizofanyika kupitia mchango wake wa Awali alioutoa hapo mwanzoni.
Baada ya kuwasili eneo hilo Mhe. Rweikiza amefurahishwa na jinsi mchango wake wa Shilingi Laki Nne ulivyosaidia na hivyo kutoa Milioni 8 ambazo zitasaidia kuendeleza Ujenzi wa jengo hilo na kulifanya liwe la Kisasa.
Mchango huo unakuja siku chache zikiwa zimesalia kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2021ambapo wanawake Kijiji hicho wamekuwa wakitembea umbali wa Km 6 kufuata Kliniki kwenye Zahanati ya Kijiji, na hivyo kwa nyakati tofauti wakashukuru ujio wa Mbunge kufika kijijini hapo.
Mhe. Rweikiza amekamilisha Ziara yake ya Siku ya kwanza Tangu kuchaguliwa kwa Kufika Kata Kagya ambapo pamoja na Mambo mengine ametoa Shilingi Milioni 12 kwa ajili ya Ujenzi wa Daraja la Omkibimbili ambalo limekuwa Kero kipindi cha Mvua, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aloitoa wakatti wa kuomba ridhaa Mwaka Jana.
Sambamba na hilo Mhe. Rweikiza amekamilisha ahadi yake ya Kulipa mshahara wa walinzi wawili jumla ya Shilingi laki Tano na kabla ya kuondoka Kata hiyo amefika Shule ya Sekondari Kibirizi na huko kuwashukuru na kuwaachia laki Mbili ya Sukari na Mipira miwili.