Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama akizungumza na walimu wakuu, Maafisa Elimu Kata na Walimu wa Taaluma wa Shule zote wilaya ya Nyasa katika kikao kazi kilichofanyika Ukumbi wa Kassim Majaliwa Uliopo Mbamba bay Sekondari katika kikao kazi Chenye lengo la kuboresha Utendaji kazi na kuinua taaluma Wilayani Nyasa.
………………………………………………………………………….
Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma leo, imefanya Kikao kazi cha Siku moja Kwa Walimu wakuu, walimu wa Taaluma na Maafisa Elimu kata, kikao chenye lengo la kuwajengea Uwezo washiriki hao kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Mafunzo yamefanyika katika Ukumbi wa Kassim majaliwa uliopo katika Shule ya Sekondari Mbamba bay, ilyopo katika Kijiji cha Ndengere Kata ya Mbamba bay Wilayani Hapa.
Akifungua Kikao kazi, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama amewataka Washiriki kuwaandaa wanafunzi kwa kuwafundisha mada zote, zinazotakiwa kufundishwa ili kuwaandaa vema na mitihani ya kiwilaya na kitaifa ili kujiepusha na Udanganyifu katika kipindi cha Mitihani.
Ameongeza kuwa kuwaandaa wanafunzi vizuri, kwa kuwafundisha mada zote, anazotakiwa kufundisha kwa mwaka mzima, na mazoezi ya mara kwa mara ni njia pekee ya kuhakikisha wanafunzi wanafaulu, kwa kiwango cha juu na kuandaa wataalam wazuri watakaojenga Taifa la Tanzania kwa miaka ijayo, waliondaliwa vizuri na kufaulu mitihani.
Aidha amesema Halmashauri itawachukulia hatua za kinidhamu na Kisheria mwalimu yeyote atakayesababisha, aidha kushusha taaluma Wilayani hapa au kusababisha udanganyifu wa Mitihani yote ya Ndani ya Wilaya, Mkoa na kitaifa.
“ndugu Walimu nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya, na kuhakikisha Wilaya ya Nyasa inafaulisha wanafunzi. Nachukua Fursa hii kuwataka kutekeleza majukumu yenu vizuri, kwa kuwafundisha wanafunzi mada zote unazotakiwa kufundisha na kujiepusha na Udanganyifu wa Mitihani, kwa kuwa umewaandaa vizuri wanafunzi wako. Mimi kama mwajiri wenu nimewaita ili kuwakumbusha kutekeleza majukumu yenu, katika Shule zenu kwa kuwa kazi ya mwalimu ni kufundisha na wanafunzi wafaulu Mitihani. Aidha sitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa walimu ambao hawatatekeleza kwa majukumu yao”
Awali Ofisa Elimu Msingi wilaya ya Nyasa Bw. Said Kalima, akitoa Takwimu za Ufaulu Wilaya ya Nyasa kwa Miaka Miwili Mfululizo, amesema wilaya imepanda, kwa ufaulu kwa darasa la nne, kwa mwaka 2019 wilaya ilipata wastani wa asilimia 96.2, na mwaka 2020 tulikuwa na wastani wa 96.4, na darasa la saba wilaya kwa mwaka 2019 ilikuwa na wastani wa asilimia 78.81 na kwa mwaka 2020 wilaya imepata wastani wa asilimia 83.2 na kusema haya ni mafanikio makubwa sana yaliyofanywa na walimu wa Nyasa na kuwapongeza kwa uchapakazi wao.
Aidha amewataka Walimu hao kuongeza juhudi za kufundisha kwa kumaliza mada ili kuendelea kupandisha ufaulu na kufikia asilimia 100, kwa mwaka 2021, kwa kuwa matokeo ya mwaka jana yameshapita hivyo kwa sasa ni maandalizi ya kuongeza ufaulu kwa mwaka huu, hivyo kuna kila sababu ya kukumbushana.
Bw Kalima amesema kuwa ili kuboresha Utendaji kazi wa Viongozi kwaka 2021, Idara ya Elimu Msingi imewaandalia mkataba maalum kati ya Viongozi hao wa kata na Shule ili kuwapima kwa malengo waliyopewa, na jinsi alivyotekeleza. Aidha kwa ambaye hatatekeleza mkataba huo atachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema Kikao kazi hicho kimewakumbusha majukumu yao, na watayatekeleza ili kuifanya Wilaya ya Nyasa iwe juu kwa kuwaandaa wahitimu wenye Taaluma bora na kuleta Tija katika Taifa la Tanzani.
Imeandaliwa na Netho C. Sichali
Afisa habari Nyasadc
0767417597