Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya (kulia) akiwasilikiliza time kutoka Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Kilimo cha Kitropiki IITA walipokutana leo katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Mjini Dodoma kuutambusha uongozi mpya wa shirika hilo.
………………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ameliomba Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Kilimo cha Kitropiki IITA kuongeza na kuimarisha maeneo ya ushirikiano na Serikali hasa katika maeneo ya Upimaji wa afya ya udongo, kilimo cha kibiashara, elimu na mapambano dhidi ya sumukuvu.
Akionge leo wakati wa mkutano na Shirika hilo katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Katibu kuu amesema bado kuna changamoto katika maeneo hayo hivyo ni vyema Shirika hilo kuongeza nguvu katika kutatua changamoto katika maeneo hayo ya ushirikiano.
Aidha amesema Serikali inatilia mkazo Wakulima kulima kibiashara ili kuongeza kipato hivyo shirika la IIITA linaweza kuendelea kusaidia kufundisha teknolojia rahisi za kilimo ili mkulima apate manufaa zaidi.
“Tunataka mabilionea wa Tanzania watokane na Kilimo, katika kufanikisha hilo ni lazima tuongeze uwekezaji kwenye sekta hii ili wakulima wetu walime kibiashara,waweze kutumia teknolojia rahisi kugundua magonjwa na namna ya kuyadhibiti na weweze kuwasiliana na soko kwa wakati muafaka” alisema Gerald Kusaya.
Hata hivyo Katibu Mkuu ameeleza jitihada za Serikali za kupima afya ya udongo kwa kila Kata ili wakulima kujua aina ya udongo na mbole zitakazohitajika hivyo kuliomba shirika hilo kuendelea kutoa ushirikiano utakao saidia upatikanaji wa vifaa vya kupimia udongo.
“Kinachowakwamisha wakulima wengi ni kujua tabia za udongo wanaoutumia katika kilimo, serikali imejipanga kugawa vipima udogo kwa maafisa ugani ili waweze kuwashauri wakulima ipasavyo, lakini kulingana na uwepo wa hamashauri nyingi nchini shirika hili linaweza kusaidiana na serikali katika upatikanaji wa machine hizo” alisistiza Gerald Kusaya.
Katibu Mkuu alimalizia kwa kusema Wakulima bado wanahitaji elimu ya uhifadhi baaada ya mavuno ili kuwasidi kupunguza upotevu wa mazao yao na kuepuka matatizo ya sumukuvu hivyo kushauri shirika hilo kuimarisha mashirikiano katika mapambo dhidi ya sumuku na uhifhadi baada ya kuvuna.
Akionge wakati wa wasilisho la malengo na mafanikio ya Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Kilimo cha Kitropiki Mkukurungenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt. Leena Triphath amesema Shirika lipo tayari kuendelea kushirikana n serikali katika maeneo mbalimbali ya kiutafiti kwa kuwa lengo ni kuwasaidi wakulima wadogo.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba Shirika limefanikiwa kuwa na miradi mingi nchini Tanzania ikiwepo ya utafiti wa mihogo, Migomba , mazao ya mikunde, kupambana na magonjwa ya mihogo,kupambana sumukuvu na kusomesha wataalamu.
Mkurugenzi huyo alimalizia kwa kumbuomba Katibu Mkuu kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo ya upatikanaji wa vibali vya watafiti wao kuishi hapa nchini jambo ambalo Katibu mkuu aaliwaahidi kusaidia watakapolileta kwa njia ya maandishi.
Akitoa maoni yake Mkuu wa Kitengo cha sheria wizarani hapo Bw. Obadia Kamea amesema wizara ilikuwa na makubaliano ya kisheria na shirika hilo ambpo walikuwa wakipata msamaha na wepesi wa upatikanaji wa vibali vya kuishi nchnini lakini baada ya madiliko ya sheria msamah huo ukafutika.
Bwana Kamea amewashauri shirika hilo kwa kushrikiana na wizara kukutana na kuboresha bakubaliano hayo ili ni yaweze kuendana na sheria ya sasa.
Mwisho.