Home Mchanganyiko NYUMBA 62 ZAEZULIWA MAPAA NA UPEPO

NYUMBA 62 ZAEZULIWA MAPAA NA UPEPO

0

**********************************

Na Zillipa Joseph     Katavi

Mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika manispaa ya mpanda mkoani katavi imepelekea jumla ya nyumba 62 za kata ya Ilembo; kuezuliwa mapaa huku nyingine zikibomoka na kuacha kaya 17 zikiwa hazina makazi; na kuharibu vibaya mazao yaliyopo katika mashamba

Mtendaji wa Kata ya Ilembo bwana Emily Katendele amesema mvua hiyo ilinyesha alfajiri ya kuamkia tarehe 20 February mwaka huu

Katendele amefafanua kuwa kufuatia uharibifu huo kaya 17 zimepoteza makazi ambapo kaya 13 zinatoka katika mtaa wa Ilembo na kaya 4 zinatoka mtaa wa Mapinduzi

Aidha aliongeza kuwa sababu kubwa ya uharibifu huo ni ujenzi wa nyumba bila uwekaji lenta huku nyumba nyingi zikiwa zimejengwa kwa kutumia matope badala ya saruji

Pia amewataka wakazi wa eneo hilo kujenga mazoea ya kupanda miti ili iwasaidie kukinga upepo dhidi ya nyumba zao

wakizungumzia hali ilivyokuwa baadhi ya waathirika Evarist Saninga,Victory Mfinula na Hosias Mbwilo wamesema mvua hiyo ilianza na upepo mkali kisha kufuatiwa na matone makubwa ya mvua na barafu vipande vipande akiwemo

‘Kwa kweli mvua kama hiyo hatujawahi kuiona kama kwangu nilikuwa nikikusanya barafu na kumwaga zinajaa ndoo’ alisema Saninga

Hivi unanvyoniona niezidi kuwa na maisha magumu baada ya nyumba kuezuliwa vyumba vyote, hapa nalia lia tu kheri Mungu angenichukua’ alisema Mzee Mfinula mzee maarufu mwenye umri wa miaka 84 ambaye pia ni Mzee wa kimila wa kabila la Wabende

Naye Mbwilo aliyekuwa na jeraha mguuni amesema ukuta ulimdondokea akiwa katika harakati za kuwatoa watoto wake nje ya nyumba

Wajumbe wa serikali ya mtaa wa Ilembo wakiwa wameambatana na viongozi mbalimbali wamepita kutoa pole kwa waathirika wa mvua hiyo ambapo Mbunge wa Jmbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi ametoa fedha kwa ajili ya chakula, mabati, ufundi, tofali na kujenga upya nyumba zilizoathirika

“Niliposikia habari hizi niliguswa na kuamua kuja kujionea mwenyewe, kama ulivyoshuhudia kuna ambao wanahitaji msaada wa haraka” alisema Kapufi

Ameeleza kuwa atalifikisha suala hilo katika vyombo husika vinavyoshughulika na majanga

Kwa kuanzia nimeona nitumie fedha yangu kuwasaidia maana baadhi yao wanaishi kwa majirani na wengine vyakula vyao vimelowa na maji, alisema

Aidha mvua hiyo pia imeharibu vibaya mazao yaliyokuwa mashambani kama mahindi, migomba na mbogamboga