Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akimkabidhi Mratibu wa Kituo cha Afya ya Mimea Kanda ya Kati (Dodoma) Bi. Happiness Lota barakoa maalum (Flits mask) kama sehemu ya vitendea kazi vitakavyotumika katika majukumu yao ya kila siku ya kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea katika ofisi za Wizara ya Kilimo Makao Makuu Jijini Dodoma leo tarehe 22 Februari, 2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akimkabidhi Mtumishi wa Kituo cha Afya ya Mimea Kanda ya Kati (Dodoma) Bwana Laurent Kazumba (Koti maalum – Ovarall) kama sehemu ya vitendea kazi vitakavyotumika katika majukumu yao ya kila siku ya kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea katika ofisi za Wizara ya Kilimo Makao Makuu Jijini Dodoma leo tarehe 22 Februari, 2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akimkabidhi Mtumishi wa Kituo cha Afya ya Mimea Kanda ya Kati (Dodoma) Bi. Kissa Mwamala (Miwani maalum) kama sehemu ya vitendea kazi vitakavyotumika katika majukumu yao ya kila siku ya kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea katika ofisi za Wizara ya Kilimo Makao Makuu Jijini Dodoma leo tarehe 22 Februari, 2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akimkabidhi Mtumishi wa Kituo cha Afya ya Mimea Kanda ya Kati (Dodoma) Benis Yusuph vifaa vya kukinga vidole (Gloves) kama sehemu ya vitendea kazi vitakavyotumika katika majukumu yao ya kila siku ya kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea katika ofisi za Wizara ya Kilimo Makao Makuu Jijini Dodoma leo tarehe 22 Februari, 2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akimkabidhi Mratibu wa Kituo cha Afya ya Mimea Kanda ya Kati (Dodoma) Bi. Happiness Lota viatu vigumu (Gum boots) kama sehemu ya vitendea kazi vitakavyotumika katika majukumu yao ya kila siku ya kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea katika ofisi za Wizara ya Kilimo Makao Makuu Jijini Dodoma leo tarehe 22 Februari, 2021.
*************************************
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya leo mchana tarehe 22 Februari, 2021 amekabidhi vitendea kazi kwa Watumishi wa Afya ya Mimea Kanda ya Kati vyenye thamani ya shilingi milioni 3,688,800.
Makabidhiano ya vitendea kazi hivyo yamefanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ambapo awali Katibu Mkuu amesema ametoa vitendea kazi hivyo mara baada ya kuwatembelea mwaka jana na kumueleza kuwa wamekuwa wakikabiliwa na ufinyu wa bajeti ya ajili ya kununua vitendea kazi hivyo.
Mratibu wa Afya ya Mimea Kanda ya Kati Bi. Happiness Lopa amemshukuru Katibu Mkuu wa kutimiza ahadi yake na kuahidi kuwa vitendea kazi hivyo vitatumika sawasawa na kusudio lake.
“Kwa niaba ya Watumishi wenzangu wa Kituo cha Afya ya Mimea Kanda ya Kati namshukuru Katibu Mkuu wa kununua vitendea kazi hivi; Ambavyo tutavitumia kwa ajili ya kutekeleza majukumu yetu ya kazi za kila. Vifaa hivi ni muhimu katika kutimiza jukumu moja kati ya majukumu yetu ya kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea kama panzi aina ya nzige, ndege na panya.”
Vitendea kazi vilivyokabidhiwa na Katibu Mkuu kwa Watumishi hao ni pamoja na viatu vigumu (Gum boots) 10, makoti maalum (Overall) 10, vifaa vya kukinga vidole (Gloves) 20, barakoa maalum (Flits mask) 9, miwani maalum 10, makoti maalum (Reflector jacket) 20 na makoti ya mvua (Rain coat) 10.