Mwenyekiti mpya wa Chama cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA) Hassan Hassanoo kulia akizungumza jambo katika katika uchaguzo huo ambapo aliweza kuibuka na ushindi baada ya kupata kura 15 dhidi ya mpinzani wake ambaye alipata kura 14 kushotoka kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uchaguzi huo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uchaguzi huo mkuu wa Chama cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA) akitoa hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano huo.
********************************
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
CHAMA cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA) hatimaye kimepata safu yake mpya ya uongozi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Wilayani Bgamoyo ambapo katika nafasi ya Mwenyekiti imechukuliwa na Othuman Hassan Hassanoo kwa kuibuka na ushindi kwa kupata kura 15 akifuatiwa na mpinzani wake Robert Munisi ambaye alipata kura 14 kati ya 32 zilizopigwa.
Katika uchaguzi huo ambao ulikuwa wa vuta ni kuvute na ushindani mkali ukilinganisha na chaguzi nyingine zilizopita katika miaka ya nyuma uliweza kusimamiwa vilivyo na Shirikisho la soka Tanzania (TTF) chini ya Mwenyekiti wa uchaguzi huo Kiomoni Kibamba ambaye aliweza kuendesha zoezi hilo kwa kuzingatia sheria na taratibu zote za mchezo wa soka.
Mwenyekiti huyo mpya wa Corefa ambaye amefanikiwa kutetea kiti chake katika kivumbi hicho cha uchaguzi aliweza kupata kura 15 za ndiyo, na kura 14 za hapana huku kura tatu zikiwa zimeharibika huku mpinzani wake wa karibu Robert Munisi alipata kura 14 za ndiyo huku kura 15 za hapana na tatu zikiharibika.
Upande wa nafasi ya Makamu mwenyekiti ilinyakuliwa na Ibrahim Gama ambaye alijizolea kura zipatazo 23 , huku nafasi ya Katibu Mkuu ikienda kwa mwandishi wa michezo wa zamani wa Gazeti la Tanzania daima Athuman Masenga aliyepata kura ziapatazo 15 huku mpinzani wake Frorence Ambonisye akipata kura 14.
Kwa upande wa nafasi ya Katibu Msaidia ilikwenda kwa Hafidhi Konyamale aliyepata kura 17 huku mpinzani wake Charles Ndagala akijinyakulia kura 12 huku nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu ikienda kwa Priscus Miyangu aliyepata kura 11, huku nafasi ya Mweka hazina ikienda kwa Mohamed Ally aliyepata kura 18 za ndiyo na mpinzani wake Bernard Yombayomba akipata kura 11.
Katika nafasi ya Mwakilishi wa vilabu ilinyakuliwa na mtangazaji kutoka shitika la utangazaji TBC Jesse John ambaye aliibuka kidedea baada ya kuinyakulia kura zipatazo 18 za ndiyo huku mpinzani wake Ramadhani Lukanga akiambulia kura 10.
Kwa upande wa nafasi Kamati ya utendaji zilinyakuliwa na Siman Mbelwa, Godfrey Haule , pamoja an Abdul Pyala, ambapo kwa wakilishi wa soko la wanawake ilikwenda kwa Faraja Makale.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni ambaye pia alikuwa Mgen rasmi katika uchaguzi huo wa Corefa aliwapongeza viongozi wapya waliochaguliwa na kuwataka kuungana kwa pamoja katika kukuza mchezo wa soka nadani ya Mkoa wa Pwani sambamba na kuelekeza nguvu zao katika kuisaidia timu ya Bagafriends ambayo ni mabingwa wa ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa.
Uongozi wa cha kuhakikisha kwamba inawekeza zaidi katika kuzisaidia timu mbali mbali mbali za soko ambazo zinakuwa zikiwakilisha katika michuano mbali mbali ili ziweze kufanya vizuri na kuuletea heshima Mkoa wa Pwani katika sekta ya michezo.
Aidha Mgeni aliongeza kuwa vyama vya soka husika vinatakiwa kuweka mikakati kabambe ambayo ni endelevu katika kuanzia programu maalumu kwa ajili ya kukuza vipaji kwa wachezaji wadogo pamoja na kuzipandisha daraja timu mbali mbali ambazo zinashiriki katika ligi tofauti.
“Kikubwa ninachowaomba viongozi tusigeuze changamoto ya timu zetu kwa lengo la kuweza kujinufaisha sisi wenyewe na kwamba wahakikishe wanashirikiana na wadau wa mchezo wa soko katika kuwekeza nguvu zao katika kuzisaidia timu amabzo zinakuwa zinawakilisha Mkoa ili wachezaji waweze kucheza katika mazingira ambayo ni rafiki,”alisema Mgeni.