rais wa chama cha wataalamu wa maendeleo ya jamii Tanzania (CODEPATA) Bw. Wambura Sunday,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu Kongamano la CODEPATA unaotarajiwa kufanyika Februari 24 jijini Dodoma ambapo zaidi ya wataalamu wa maendeleo ya jamii takribani 400 kukutana.
Katibu Mkuu wa CODEPATA Bw. Pascal Mahinyila,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu walivyojiandaa ili kufanikisha Kongamano la CODEPATA ambao utawakutanisha wa wataalamu wa maendeleo ya jamii takribani 400 nchi nzima Februari 24,2021 jijini Dodoma .
Mratibu wa CODEPATA kanda ya ziwa ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa chama hicho Bi. Aliadina Peter,akitoa ufafanuzi juu ya lengo la kongamano hilo litakalofanyika Februari 24,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Chama cha wataalamu wa maendeleo ya jamii Tanzania (CODEPATA) kinatarajia kuwakutanisha wataalamu wa maendeleo ya jamii takribani 400 nchi nzima katika kongamano kubwa lenye lengo la kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo.
Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 22,2021 jijini Dodoma na rais wa chama cha wataalamu wa maendeleo ya jamii Tanzania Bw. Wambura Sunday amesema kongamano hilo ni muhimu kwa sababu litawakutanisha wataalamu wa maendeleo ya jamii kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni kushirikishana mbinu na mikakati itakayowezesha kutekeleza majukumu yao.
Ttutakutanisha wanachama wa chama cha wataalamu wa maendeleo ya jamii ili kupeana mbinu na mikakati itakayowezesha kutekeleza majukumu yetu kwa ufasaha Zaidi pia kubadilishana uzoefu na mbinu mpya” amesema Bw. Wambura.
Amesema Pamoja na maada mbalimbali zitakazowasilishwa katika kongamano hilo pia kutakuwa na maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na vikundi mbalimbali vya wajasiliamali, watu binafsi, asasi za kiraia na taasisi.
“Tutawasilisha maada mbalimbali na majadiliano ambapo maada sita (6) zitawasilishwa na kujadiliwa wakati wa kongamano kati ya maada sita maada tatu zitawasilishwa katika majadiliano ya vikundi” amesema.
Ameongeza kuwa “Pia tutazindua tovuti ya chama, uchaguzi mkuu wa chama kuchagua rais, Makamu wa rais, kstibu wa chama, mweka hazina na waratibu wa kanda 7” amesema.
Amesema Katibu Mkuu Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na Watoto idara kuu ya maendeleo ya jamii atawasilisha maada kuu kuhusu uongozi wa kimkakati katika kutekeleza na kusimamia shughuli za maendeleo ya jamii hapa nchini
Amesema mkutano huo ni mkutano wa nne ambapo mikutano mitatu imeshafanyika wakishirikiana na Wizara ya Afya tangu mwaka 2017 ikishirikisha Sekretarieti za Mkoa, Mamlaka za serikali za mitaa, taasisi za Wizara na Wizara za kisekta na Asas za kiraia.
Amesema kwa muda mrefu sana wamekuwa wakifanya shughuli mbali mbali za maendeleo ya kijamii lakini bado hazijatambuliwa na jamii lakini wamekuwa na mchango kubwa sana hasa katika kuhamasisha vikundi katika maeneo yao.
Amesema kongamano hilo litakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo “wataalamu wa maendeleo ya jamii ni nguzo ya kujenga jamii yenye kujitegemea katika kuimarisha uchumi wa kati”.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CODEPATA Bw. Pascal Mahinyila amesema chama hicho kilianzishwa rasmi mwaka 2017 na kusajiliwa rasmi mwaka 2019 sambamba na kuweka miongozo mbalimbali katika kuendesha taaluma hiyo.
Nae Mratibu wa CODEPATA kanda ya ziwa ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa chama hicho Bi. Aliadina Peter amesema walianzisha chama hicho kwa lengo la kusimamia taaluma hiyo iweze kufanya vizuri katika kutekeleza majukumu ya taaluma ya maendeleo ya jamii.