……………………………………………………………………………………………
NA DENIS MLOWE,IRINGA
Kampuni ya Kamal Group ya Jijini Dar es Salaam imetoa miguu bandia yenye thamani ya mamia ya mamilioni ya shilingi kwa watu 51 wenye ulemavu wa viungo na kuwalejeshea furaha ambayo hawakutarajia kutokana na gharama kubwa za viungo hivyo bandia.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo kwa wahusika, Mratibu wa kampuni hiyo, Stela Nyaki katika makabidhiano yaliyofanyika katika ukumbi wa Hallfear mbele ya mbunge wa viti maalum Ritta Kabati aliyesababisha kupewa viungo hivyo alisema kampuni hiyo inaamini kuwa inao wajibu wa kusaidia maendeleo ya jamii inayoizunguka.
“Tunaamini kuwa ni wajibu wetu kusaidia jamii inayotuzunguka ni wajibu wetu kuleta tabasamu katika nyuso za watu wanaotuzunguka na kuhakikisha kuwa wale wenye ulemavu wa miguu wanaweza kutembea tena,” alisema
Alisema lengo la Kamal Group ni kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanarudi katika sehemu zao za kazi ili watoe michango yao katika kuijenga Tanzania. Kwa vile tunacho kiwanda chenye zana za kimataifa hapa hapa nchini Tanzania.
Alisema kuwa kampuni hiyo imewezesha walemavu 51 kuweza kupatiwa Miguu ya kisasa ya Bandia ambayo inakadiriwa Mguu mmoja unagharimu kiasi cha shilling million 2 hadi 3 ambapo yote kwa pamoja lakini kwa jitiada za mbunge wa viti maalum Ritta Kabati wamepatiwa Miguu hiyo Bure kutoka Kamal Group.
Baadhi ya Walemavu waliopatiwa Miguu hiyo wamemshukuru mbunge Ritta Kabati na kampuni ya Kamal Group kwa moyo wa pekee wa kuwajali wananchi wake kwa kuzingatia makundi yote kwenye jamii ambapo wamesema kwa sasa wataenda kufanya kazi na kuachana na utegemezi.
Aidha wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwezesha kampuni ya Kamal Group kuweza kumuunga mkono rais John Magufuli kutimiza maono yake ya kuwawezesha walemavu kupata miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za kujiingizia kipato cha kila siku.
Naye mwenyekiti Chama Cha Walemavu Tanzania (Chawata) mkoa wa Iringa,Shaban Shomari alisema bei ya mguu mmoja bandia kwa sasa inafikia Shilingi milioni mbili Hadi nne na hivyo kuwafanya watu wengi washindwe kumudu.
“Na ndio maana tunaishukuru sana kampuni ya Kamal kwa msaada huu na tunaomba makampuni mengine nayo yawaige,” alisema.
Kwa upande wake Mbunge wa viti Maalum Ritta Kabati licha ya kuishukuru kampuni ya Kamal Group kuwapatia walemavu miguu hiyo atahakikisha walemavu wote wanafikiwa ili kuwalejeshea furaha na kuwafanya waweza kuendelea na majukumu yao ya kila siku.
Alisema kuwa hii awamu ya pili kwa kampuni hiyo kutoa msaada wa miguu bandia hivyo kama mbunge atahakikisha anawesema bungeni walemavu wote ili waweza kupata misaada zaidi na kutoa wito kwao kufanya kazi kwa bidii kuleta maendeleo ya nchi na yao kwa pamoja.