Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AWATAKA WALEMAVU KUTOKUWA WANYONGE

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AWATAKA WALEMAVU KUTOKUWA WANYONGE

0

Mbunge wa Viti Maalum MKoa wa Iringa Rita Kabati akizungumza wakati wa kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye hafla ya kukabidhi miguu bandia kwa watu wenye ulemavu Mjini Iringa.

Naibu waziri Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Mratibu wa zoezi la upimaji na ugawaji wa miguu bandia kwa watu wenye ulemavu kutoka Kamal Group Stella Nyaki akizungumza kwenye Hafla hiyo

Naibu waziri Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa tatu kulia) akimkabidhi Miguu bandia kwa watu mwenye ulemavu wakati wa hafla ya kukabidhi miguu bandia kwa watu wenye ulemavu wa Mkoa wa Iringa. (wa kwanza kulia) ni Daktari Kiongozi wa Kamal Group Naresh Trived, (wa pili kulia) ni Mbunge Viti maalu Mkoa wa Iringa. Rita Kabati, na (wa kwanza Kushoto) ni Mratibu wa zoezi hilo kutoka Kamal Group Stella Nyaki.

Baadhi ya watu wenye ulemavu waliohudhuria Hafla hiyo wakifuatila hotuba ya Mgeni rasmi.

………………………………………….

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu Ummy Nderiananga amewata watu wenye ulemavu kutokuwa wanyonge kwani wao ni kundi katika jamii wanaoweza kazi na kuendesha maisha yao.

Mh. Nderiananga aliyasema hayo Mjini Iringa wakati wa hafla ya kuwakabidhi miguu bandia walemavu 51 katika Ukumbi wa Orofea uliopo Manispaa ya Iringa ambapo alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo.

Mh. Nderiananga alisisitiza kuwa walemavu siyo watu wadhaifu bali wana uwezo wa kufanya shughuli yeyote kwa ufanisi kama watu wengine hivyo kuishukuru kampuni ya Kamal waliowezesha zoezi hilo na kwamba itawasaidia kuweza kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kuwaongezea kipato.

“Watu wenye ulemavu wanauwezo wa kujisimamia wenyewe kwa kufanya shughuli zao za kiuchumi na kuendesha maisha yao hivyo nawasihi sana Ndugu zangu wenye ulemavu msiwe wanyonge unaweza kufanya kitu na hata kumuajiri mtu mwingine” alisema Mhe. Nderiananga.

Aidha waziri aliishukuru kampuni ya Kamal kwa moyo wa upendo waliouonyesha na kurudisha matumaini yaliyopotea kwa walemavu hao.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Dkt. Rita Kabati ambaye ameratibu zoezi zima la kuwakusanya watu wenye ulemavu manispaa hiyo alisema kuwa anatambua na kuthamini mchango wa watu wenye ulemavu nakwamba anaamini kwa kupatiwa miguu bandia itaongeza chachu ya wao kuwapa uwezo wa kujisimamia kwenye shughuli zao.

Aidha Mhe.Kabati ameishukuru kampuni ya Kamal group kwa moyo wao wa kipekee kwa huduma nzuri ya kuwapima na kuwapatia viungo bandia watu wenye ulemavu zaidi ya 50 Katika manispaa ya Iringa.

Aidha Dkt. Kabati ameongeza kuwa kwa kutambua mchango wa kundi hilo maalum ameanzisha NGO Maalum itakayofanyakazi kwenye Mikoa ya nyanda za juu kusini kwaajili ya kushughulikia matatizo ya watu wenye ulemavu sambamba na kuwapatia mahitaji yao ya kijamii.

“Mhe. Naibu waziri Katika kutambua umuhimu wa watu wenye ulemavu nimeanzisha NGO itayoshugulikia masuala ya walemavu kwenye Mikoa ya Nyanda za juu kusini na kuwapatia nahitaji yao ya kijamii ili waweze kuendeleza maisha yao” alisema Mhe. Kabati.

Kwa upande wake Mratibu zoezi hilo kutoka Kamal Group ya Jijini Dar es Salaam Stella Nyaki alisema kuwa Kampuni yao tayari wamekwishatoa vifaa zaidi ya 3500 na wanatarajia kugawa vifaa 2500 kwa kipindi hiki na kwa Manispaa ya Iringa wametoa vifaa 51 na kuwapima walemavu 32.