Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Zainabu Kawawa akizungumza katika kikao maalumu alichokiitisha kwa ajili ya kuweza kukutana na wadau mbali mbali wa michezo kwa ajili ya kujadili na kuweka mikakati ya kutafuta fedha na vifaa ili kuisaidia timu ya soka ya Bagafrieds ambayo inashiriki michuano ya mabingwa wa mkoa ngazi ya Taifa.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni akizungumza jambo katika kikao hicho ambacho kiliitishwa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kwa lengo la kuweza kuona namna ya kupanga kuisaidia timu hiyo ya Bagafrieds ambao ndio wawakilishi pekee wa Mkoa wa Pwani katika ligi ya mabingwa ngazi ya Taifa.
Baadhi ya wadau wa mcheozo wa kandanda Wilaya ya Bagamoyo ambao walihudhulia katika kikao hicho wakiwa wanachangia fedha kwa ajili ya kuisaidia timuya Bagafriends ili iweze kufanya vizuri katika michuano hiyo ngazi ya Taifa.
……………………………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Zainabu Kawawa katika kuunga mkono juhudi za kukuza sekta ya michezo ametoa sapoti kwa kuchangia kiasi cha shilingi laki tatu kwa kikosi cha timu ya soka ya Bagafriends ambayo ni mabingwa wa Mkoa wa Pwani katika michuano ya ligi daraja la tatu ambayo kwa sasa inajiandaa na kivumbi cha ligi ya mabingwa wa mikoa ngazi ya Taifa inayotarajia kuazna kutimua vumbi lake mwishoni mwa mwezi huu 2021..
Kawawa ametoa mchango huo wakati alipokutana na viongozi mbali mbali wa mchezo wa soka wa Wilaya ya Bagamoyo,viongozi pamoja na wadau wengine wa michezo lengo ikiwa ni kukutana kwa ajili ajili ya kujadli na kupanga mikakati ambayo itasaidia timu hiyo iweze kufanya vizuri sambamba na kuchangisha fedha ambazo zitasaidia wachezaji katika kipindi cha ligi hiyo ngazi ya Taifa.
Pia Kawawa amewaomab wadau mbali mbali wa michezo katika Wilaya ya Bgamoyo pamoja na Pwani kwa ujumla kushikamana kwa pamoja katika kuisaidia kwa hali na mali timu hiyo ili iweze kutimiza malengo yake yakuweza kufanya vizuri katika ligi hiyo na kupanda daraja katika msimu unaokuja.
“Hii ni timu yetu ya Bagafriends kwa hiyo mimi kaka mkuu wa Wilaya ninawaomba wadau wa mchezo wa soka ndani ya Bgamoyo pamoja na Mkoa wa ujumla tushikamane kwa pamoja kwa ajili ya kuipa sapoti ya kuisaidia michango mbali mbali ili wachezaji ambao wanaunda timu hii waweze kucheza kwa molali zaidi na kutuwakilisha vema katika michuano ya ngazi ya Taifa,”alifafanua Kawawa.
Kadhalika aliwaasa viongozi wa mpira wa soka katika Wilaya ya Bagamoyo kuweka mipango kabambe ya ambayo itaweza kufanikisha kupatika kwa ushindi wa timu hiyo ya Bagafriends lengo ikiwa ni kufanya vizuri zaidi katika michuano hiyo ya ngazi ya Taifa na kuongeza kuwa kwa sasa timu hiyo inatakiwa mahitaji mbali mbali ya msingi ikiwemo vifaa, fedha, mipira pamoja mambo mengine.
Pia Mku huyo aliongeza kwamba katika kuhakikisha kwamab sektya ya michezo inaendelea zaidi serikali ya Wilaya ya Bgamoyo itaendelea kushirikiana bega kwa bega wadau tofauti katika kuhakikisha kwamba timu ya bagafriends inaweza kufika mbali na kuibuka na ushindi katika kila mchezo lengo ikiwa ni kuipeperusha vema Wilaya ya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani.
Aidha aliwataka wachezaji wote ambao wanaunda timu hiyo ya Bagafriends kuwa na bidii katika michezo yote na kuwa na nidhamu ya mchezo pindi wanapokuwa uwanjani na kuzingatia sheria zote 17 za mchezo wa soka na kwamba ataendelea kuwapa sapoti mbali mbali kutoka kwake ili kuweza kutmiza malengo amabyo wamejiwekea.
“Hii timu kwa sasa ndio wawakilishi pekee wa Mkoa wa Pwani katika ngazi ya Taifa kwa hivyo hatuna budu wote kwa pamoja tukawa kitu kimoja bila kujali timu imetokea sehemu gani lakini tutambue kwamba ndio inauwakilisha Mkoa lakini mimi nina imani tukishikamana kwa pamoja tutaweza kuleta mabadiliko zaidi katika Nyanja ya mchezo wa soko,”alisema Kawawa.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni aliwaomba wadau mbali mbali wa mchezo wa soka katika Wilaya ya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kuungana kwa pamoja kuichangia timu hiyo ya Bagafriends ili iweze kufanya vizuri katika michuano hiyo ya michuano ya mabingwa ngazi ya Taifa.