TANZANIA imeokota pointi ya kwanza katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) baada ya sare ya 1-1 na Gambia katika mchezo wa Kundi C leo Mauritania.
Gambia walitangulia kwa bao la Momodou Bojang dakika ya 40, kabla ya Novatus Dismas kuisawazishia Ngorongoro Heroes dakika ya 87.
Tanzania iliyochapwa 4-0 na Ghana katika mechi yake ya kwanza, itakamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Morocco Jumanne ijayo kuangalia mustakabali wake wa kusonga mbele.
NGORONGORO HEROES BADO NGOMA MBICHI YATOA SARE YA 1-1 NA GAMBIA NCHINI MAURITANIA
