***********************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo horticulture yaani mboga mboga, matunda, mimea itokanayo na mizizi, pamoja na viungo (TAHA) imejipanga kuwajengea wakulima uwezo wa kulima kwa viwango vinavyotakiwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mkakati huo ulielezwa na Antony Chamanga Meneja mkuu wa maendeleo ya Asasi hiyo wakati akiongea na waandishi wa Habari kuhusiana na mwelekeo wa TAHA kwa mwaka 2021 ambapo alisema kuwa umuhimu wa horticulture umekuwa ukiongezeka siku hadi siku ambapo ili kuimarisha uwezo wao wa masoko wa kuwezesha watanzania kuuza mazao yao kwa kuwafanya walime mazao yenye viwango vinavyohitajika katika masoko.
“Ili mkulima aweze kufikia masoko hasa ya nje ya nchi ni lazima anahitaji mtu wa katika ambapo sisi kama TAHA tunajitahidi kuwaunganisha wakulima na wafanyabiashara,” Alisema Bwana Chamanga.
Alieleza pia watatilia mkazo kwenye mkubwa kwenye kilimo cha matunda aina ya Maembe, Nanasi, Parachichi na matunda mengine ambayo kwa sasa yana fursa kubwa katika usindikaji.
Alisema kuwa zao lingine watakalolipa kipaumbele ni zao la Ndizi ambapo linalimwa kanda ya kaskazini na baadhi ya maeneo ya kanda ya ziwa ambapo watahakikisha wakulima wa zao hilo wanaingia katika mnyororo wa thamani kwa kwa kuwaunganisha na wafanyabiashara.
Aidha kwa upande wa zao la pilipili alisema kuwa asilimia 90 ya ardhi ya Tanzania inakubali zao hilo ambapo pia wanajitahidi kuwaunganisha wakulima wa zao hill na masoko ya ndani na nje.
Kwa upande waka Kelvin Remen Meneja Mazingira ya Biashara wa Taha Tanzania imefanikiwa kuwa katika kiwango cha chini cha uwejaji dawa katika mazao ambapo awali kwa mwezi kulikuwa malalamiko saba ya mazao kwa mwezi kutokana na uzidishwaji wa dawa..
Alisema hivi sasa Kwa muda wa miezi Sita hadi saba kunaweza kutokea lalamiko moja tu kwani wanashirikiana na Wizara, TPRI pamoja na wazalishaji wenyewe kuhakikisha kuwa mazao hayo yanakidhi vigezo vya kupelekwa nje ya nchi.