NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe,akizungumza kwenye kikaoa mara baada ya kukutana na vyama vya msingi 41 vya Sekta ndogo ya Chai chenye lengo la kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo iliyofanyika leo Februari 19,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa kikao wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (hayupo pichani) wakati alipokutana na vyama vya msingi 41 vya Sekta ndogo ya Chai chenye lengo la kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo iliyofanyika leo Februari 19,2021 jijini Dodoma.
Mwanachama Umoja wa Wataalam wa Mifugo Wastaafu Tanzania (UWAMIWATA) Dkt.Samson Muniko akichagia mada wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe,alipokutana na vyama vya msingi 41 vya Sekta ndogo ya Chai chenye lengo la kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo iliyofanyika leo Februari 19,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu CCWT Joshua Lugaso akieleza changamoto zinazowakumba kwenye kikao na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe,alipokutana na vyama vya msingi 41 vya Sekta ndogo ya Chai chenye lengo la kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo iliyofanyika leo Februari 19,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amekutana na vyama vya msingi 41 vya Sekta ndogo ya Chai ili kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kuwa na masoko ya uhakika.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Naibu Waziri Bashe, amesema hatua hiyo imetokana na sekta ya kilimo kupata ufadhili kutoka Umoja wa Ulaya(EU) wa EURO milioni 100 ambazo kwa asilimia kubwa zinalenga kupaisha uzalishaji wa zao hilo na kuwa na tija kwa mwananchi.
Amesema serikali imeweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo kutoa tani 25000 hadi kufikia tani 60000 ifikapo Mwaka 2024 kwa kuhakikisha wakulima wanapatiwa pembejeo na uhakika wa masoko kwa njia ya mnada.
“Fedha hizo EURO milioni 48 zitajenga miundombinu ya barabara za mashambani ili kuondoa tatizo la kufikisha chai sokoni, uzalishaji w chai ni mkubwa kuliko uwezo wa viwanda vya Tanzania kuchakata chai,”amesema.
Kuhusu masoko, Bashe amebainisha kuwa tayari kuna mazungumzo yanafanyika na kampuni kubwa mbili za duniani ambzo zinanunua chai Mbombasa nchini Kenya zimekubali kufungua matawi yake ili kushiriki kwenye mnada wa chai ambao unatarajiwa kabla ya mwisho wa mwaka huu uwe umeanza.
Kadhalika, amesema ili kuondokana na tatizo la upotevu wa chai mradi huo utasaidia kujengwa kwa viwanda vidogo vya kuchakata chai karibu na mashamba ya chai.
Naibu Waziri huyo, amesema kwenye kikao hicho wamejadiliana mfumo wanaotumia wakulima kupata Pembejeo na kuwataka wakulima wote nchini kuagiza mbolea kupitia vyama vyao vya ushirika ili kupata kwa bei nafuu na kwa mkopo
Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania, Nicholaus Mauya, amesema kumekuwepo na upotevu wa chai unaotokana na kuharibika wakati wa usafirishaji na kutovunwa kutokana na kukosa viwanda vya kununua.
Amesema mkakati wa kujenga viwanda jirani na wakulima ni utaratibu unaotumika nchini India na umefanikiwa kuwa na tija.
“Uzalishaji wa chai hutegemea hali ya hewa na kuna misimu miwili ambapo uzalishaji mkubwa huwa msimu wa mvua na kusababisha chai nyingi kuharibika, kwa mfano kwa mwaka 2019/20 upotevu wa chai ulikuwa tani 2000,”amesema.
Naye, Mkulima Santino Mtenda kutoka Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, amesema iwapo soko la zao hilo likifunguliwa Dar es salaam itaokoa gharama kwa wakulima kuachana kusafirisha kupeleka Mombasa.
Amesema Wakulima wa chai wamekuwa wakigharimu hadi Sh.Milioni sita kupeleka chai Mombasa hali ambayo inasababisha wakulima kutoona tija kwenye eneo hilo.
Meneja wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja, Maduhu Mkonya amesema wamekutana wakulima hao kuhakikisha wanapata mbolea kwa kuagiza kupitia mfumo huo wa kielektroniki ambao fedha zake mkulima analipa kwa muda wa miezi 6 baada ya kuvuna mazao yake.
&&&&&&&&&