Akizungumza na waandishi wa ofisi kwake Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Sosthenes Kibwengo amesema TAKUKURU imefanikiwa kumpata mmiliki wa kampuni hiyo bw. Abubakary Kinyuma maarufu kama Abubakary Mapesa na kurejesha kiasi hicho cha fedha kwa wananchi 17 waliokuwa wamekopa katika Kampuni hiyo.
“Uchunguzi wetu umebaini kwamba baadhi ya watumishi wa Umma Wilayani Kondoa wanapokaribia kustaafu wanaotarajia kupata mafao yao ambao huchukua mikopo midogo kwenye kampuni hiyo na kulipa fedha nyingi
Bwana Mapesa ambaye amekuwa akichukua kadi zao za benki na kuzihifadhi na pindi mafao yao yanapotoka hujitwalia kiasi kikubwa cha fedha kwa riba kubwa hadi kufikia riba ya asilimia elfu 10,000″ amesema Kibwengo.
Ametolea mfano Mwalimu msitaafu mmoja alikopeshwa shilingi 350,000 lakini pamoja na kurejesha shilingi Milioni 4,600,000 pia alinyang’anywa nyumba yake yenye thamani ya milioni 37 iliyopo Ndachi Jijini Dodoma.
“Leo february 18, 2021 tunamreshejea nyumba yake na shilingi milioni moja laki nane na thelathini kwa kuwa awali alijeshewa kiasi cha shilingi milioni 2” amesema.
Aidha Kibwengo amesema kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato TanzaniaTRA wanaendelea kukokotoa kiasi cha kodi ambacho kampuni hiyo inadaiwa ambapo ilikuwa ikifanyakazi bila kulipa kodi pia wanaendelea kufuatilia wakopeshwaji 22 ambao pia wanatakiwa kulejeshewa fedha zao.
Amesema pia TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kurejesha deni la zaidi ya shilingi milioni 51 kwa chama cha akiba na kukopa cha ufundi SACCOS baada ya kuwabana wadaiwa sugu na kwa mda mrefu.
Aidha Kibwengo amewasihi wakopeshaji wa fedha Mkoa wa Dodoma kuzingatia sheria kanuni na taratibu za nchi na kuacha kuwatoza wateja wao riba kubwa na kuwataka wananchi kuwa makini na mikopo umiza na wasikubali kukabidhi kadi zao za benki kwa wakopeshaji.
Kwa upande wake mmoja wa waliorudishiwa fedha zao bw. Juma Hindo ameishukuru TAKUKURU kwa Kupambana hadi haki yao kupatikana na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya.
Amesema mnamo mwaka 2014 alikopa kiasi cha shilingi laki mbili (200,000) na ilipofika tarehe 7/1/2017 bwana Abubakary Mapesa alikwenda nyumbani kwake na mgambo na kumtaka alipe shilingi milioni 30, akatoa milioni 16 na akauza trekta kwa shilingi milioni 14 na kumkabidhi bwana Abubakary shilingi milioni 30 Cash