Na Allawi Kaboyo – Missenyi
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula amelitaka shirika la Nyumba NHC Mkoa wa Kagera kuhakikisha linamaliza ujenzi wa jengo la kitega uchumi linalojengwa Mutukula Missenyi mpakani mwa Tanzania na Uganda ili kuweka Chachu ya biashara ya mpakani kwa upande wa Tanzania.
Naibu Waziri ametoa kauli hiyo Feb 17, mwaka huu alipotrmbelea mradi huo kwa lengo la kutoka kukagua Maendeleo ya ujenzi huo na kuagiza ukamilike tarehe 15 Mach mwaka huu na kuanza kutoa huduma.
Dkt. Mabula amesema kuwa upande wa Tanzania umekuwa ukidolola kibiashara kutokana na kutokuwepo na majengo ya kibiashara hali inayopelekea watu wengi kwenda kununua bidhaa upande wa Uganda na kufanya upande huo kuchangamka.
“Mrandi huu ni wa muda mrefu na umesimama kwa kipindi kirefu hivyo niwaombe fanyeni kila kinachowezekana kufikia tarehe 15 Mach likamilike na Mimi nitakuja mwisho wa mwezi Mach kukagua” Amesema Dkt. Mabula.
Kwaupande wake Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo mhandisi Georg Shaneli amesema kuwa wapo hatua za mwisho za umaliziaji, kilichobaki ni uwekaji wa milango na madirisha ambapo amebainisha kuwa vipo vifaa ambavyo wamevisubiri kutoka nje ya nchi kwaajili ya kumaliza.
Ameeleza kuwa jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2014 na litakuwa kukamilika mwaka 2018 ambapo ameongeza kuwa ujenzi huo ulisimama kwa sababu mbalimbali Hali iliyopelekea mkandarasi aliyekuwa amepewa kazi hiyo kusimamishwa na kuanza kujengwa na NHC ambapo gharama za mradi huo ni shilingi bilioni 3 Hadi kukamilika kwake.
Meneja huduma kwa jamii wa shirika la Nyumba Muungano Saguye, amesema kuwa wameishaanza taratibu za kujenga majengo mengine katika mipaka ya Sirali na Tunduma lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara katika mipaka hiyo kwa upande wa Tanzania.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa jengo la Mutukula litawapa mwanga wa namna gani majengo mengine yatatakiwa kuwa ili kuweza kuchangamsha biashara za mipakani kw aupande wa Tanzania.