Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama akisoma taarifa ya mpango wa bajeti kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2021 katika kikao hicho cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kwa lengo la kupitisha bajeti.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani amabcho kiliandaliwa kwa lengo la kujadili mpango na bajeti kwa kipindi cha mwaka 20202 hadi 2021.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Zuberi Zwewe wa kati kati akifafanya jambo katika kikao hicho cha baraza la madiwani.
Baadhi ya waheshimiwa madiwani mbali mbali wakiwa wanafuatilia jambo katika kikao hicho cha baraza hilo amabalo limegfanyika katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kujadili mpango na bajeti katika mwaka wa 2020-2021.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe Halfani Sika wa kulia akiwa na Katibu wa Chama hicho wakiwa katika kikao kuangalia mpango wa bajeti hiyo ambayo ilikuwa ikijadiliwa na baraza la madiwani ambayo imefanikiwa kupitishwa kwa kishindo bila kupinga. Mmoja wa madiwani wa kata ya Kibuta Mhandisi Mohamed Kilumbi akiwa akichangia moja ya hoja mbali mbali amabzo zilikuwa zikijadiliwa katika kikao hicho.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
**************************************
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
BARAZA la madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani limeazima kwa pamoja kupitisha bajeti ya kiasi cha shillingi bilioni 39.8 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wake wa matumizi katika sekta mbali mbali ikiwemo miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2021 na 2022.
Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama wakati wa kikao cha baraza hilo kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya mpango na bajeti hiyo kilichohidhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali, taasisi za umma, wakuu wa idara pamoja na wakuu wa vitengo kutoka mashirika ya umma ambao walialikwa lengo la kutoa elimu kwa madiwani hao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegele amewaasa madiwani kuendelea kushikamana na kufanya kazi kwa bidii na weledi ikiwemo kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi na kuitifatua ufumbuzi lengo ikiwa ni kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika sekta mbali mbali.
Pia Jokate alisema kwamba serikali ya Wilaya ya Kisarawe itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa madiwani wote na watendaji bila ubaguzi wowote kwa lengo la kuweza kuwaletea wananchi maendeleo katika nyaja bali mbali za maji, umeme afya, na mambo mengine ya msingi kwa kuzingiatia miongozo,taratibu na sheria zote zilizowekwa za nchi.
Naye Mwenyekti wa Chama vcha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe Halfan Sika amelipongeza baraza hilo la madiwani kwa kuweza kushikamana kwa pamoja na kupitisha bajeti hiyo ambayo inakwenda kutatua au kupunguza kero na shida mbali mbali za wananchi wa maeneo mbali mbali ya Kisarawe.
Sika aliongeza kuwa lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba inaleta maenedeleo kwa wananchi wake kwa kuzingatia utakelezaji wa ilani ya cahama katika yale mambo mbali mbali amabyo yameahidiwa ili yaweze kufanyiwa kazi na kuleta mabadiliko katika Nyanja mbali mbali.
“Mimi niwapongeza madiwani wote ambao kwa kweli mmeweza kufanya kazi kwa bidii katika kuiandaa bajeti hii na kitu kikubwa ambacho tunapaswa kukifanya ni kuhakikisha tunaweka mipango yetu vizuri ya kuweza kuwatumiakia wananchi wetu ikiwemo kuwatatulia changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili na kuzitafutia majawabu kwa hivyo nina imani kupita kwa bajeti hii ni moja kati ya hatua katika maendeleo kwa wannachi wa Kisarawe.”aliafafanua Sika.
Nao baadhi ya madiwani wa baraza hilo akiwemo Adamu Nimba na Mhandisi Mohamed Kilumbi wameoumba uongozi wa halmashauri hiyo ya Ksarawe licha ya kupisha bajeti hiyo lakini waongeze ubunifu zaidi katikja suala zima la ukusanyaji wa mapato kwa kuwa ni vyanzo vingine vipya ambayo vitaweza kuisaidia kuinua kiwango cha mapato.
“Sisi kama baraza la madiwani hii bajeti tumeipitisha lakini kitu kikubwa ni lazima kujipanga zaidi na kuwatumia wataalamu wetu wa Kisarawe ambao wataweza kuzidisha kazi zaidia katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kupitia njia mbali mbali za kubuni vyavyo vipya vya muda mrefu katika ukusanyaji wa mapato hayo,”alisisitiza Adamu.
Kadhlika diwani huyo katika hatua nyingine alifafanua kwamba vyanzo vya mkaa na kuni ambavyo navyo vinatumika katika ukusanyaji mzima wa kuingiza kipato lakini vitafikia wakati vitakwisha hivyo kunapaswa kuwekwa mpango endelevu ambao utasaidia katika siku za usoni kupata suala la upatikaniji wa kuingiza mapato.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe ni miongozi mwa halmashauri tisa zilizopo katika Mkoa wa Pwani na ilianzishwa mnamo mwezi Agosti mwaka 1962,ambapo kwa mwaka huu upitishwaji wa bajeti hiyo itaweza kwenda kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kupunguza changamoto za ukosefu wa huduma mbali mbali ambazo zimekuwa zikiwakabiliwa wananchi katika maeneo yao.