**************************************
Na Ahmed Mahmoud Hai
Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameagiza Kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha inasaidiana na Mamlaka ya Mapato nchini Tra kuwakamata wafanyabiashara na wateja wanauza na kununua bidhaa bila kutoa na kudai Risiti
Aidha watu hao wamekuwa wakisababisha Serikali kukosa Mapato Stahiki na mamlaka hiyo kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji Kodi na maduhuli ya serikali
Lengai Ole Sabaya ameyasema hayo wakati wa kikao maalum na watendaji wa Tra Maafisa biashara wa halmashauri pamoja na watendaji wanaohusika na masuala ya fedha wote kwa pamoja wamejadili kuhusu kupandisha mapato ya wilaya ya Hai katika mwaka wa fedha 20020/21
Sabaya ameagiza hayo baada ya kuwepo na wafanyabiashara wachache wasio waaminifu kukwepa kulipa Kodi na kushindwa kutoa risiti kwa wateja na kuikosesha serikali mapato na kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa Kodi
Naagiza kuanzia Sasa Ocd na kamati yako ya usalama fanyeni operation ya kuwakamata wanaofanya biashara na kushindwa kutoa na kupokea risiti maana ndio wanaokosesha serikali mapato.
“Utakuta Mtu ananunua mzigo wa mamilioni ya fedha hadai risiti au anafanyia ujanja ujanja wa kupata risiti iliyoambatana na biashara iliyofanyika kamateni weka ndani tupate mapato tujenge barabara,shule, hospital tununue dawa na kuleta maendeleo kwa wananchi “Alisema mkuu wa wilaya Sabaya “
Hata hivyo Sabaya ameeleza kwamba hakuna duka lolote lillilofungwa na Mamlaka ya mapato Tra Wala akaunti za wafanya biashara Bali wafanya biashara wenyewe wamekuwa wakitoa bidhaa nje ya maduka na kuwapa wafanya biashara wadogo (machinga )wakauze nje na baadae kumletea boss faida na kupewa posho yake ya siku hivyo kusababisha Tra kukosa mapato.
Naye kaimu meneja wa Mamlaka ya mapato Tra wilayani Hai Ester Martin Mallya amesema wamekusudia kufikia kukusanya kiasi Cha shilingi bilioni 4.6 kwa mwaka wa fedha wa 2020 ,2021 ukiwa watasimamia vyema malengo walio jiwekea kwani kuna uwezekano huo na hata kuzidi malengo ya ukusanyaji wa mapato.
Amesema katika ukusanyaji wa mapato wanakutana na vikwazo vya wafanya biashara kuuza bidhaa na kuacha kutoa risiti au wakitoa wanatoa ya pesa ndogo Jambo ambalo amemuomba mkuu wa wilaya kulisimamia kwa nguvu zote waweze kufikia malengo ya ukusanyaji
Ametoa rai kwa wafanya biashara kuacha Mara moja Tabia ya kutotoa risiti na mnunuzi naye kutodai risiti kwani endapo mmoja wapo atabainika kuvunja Sheria atakumbana na faini au kifungo kwa kukosesha Mamlaka kukusanya mapato waliojiwekea
Akizungumza kwa niaba ya wafanya biashara wa wilaya hai Mwenyekiti wa wafanya biashara eneo la stand ya Boma Ng’ombe Anderson Soni ameshukuru kikao Cha pamoja na Mamlaka ya Tra na kupata mafunzo kwani wamekua wakiogopa kukutana nao na kufanya mashairiano ya juu ya kiendesha biashara.