Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wenye lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye mazao hayo nchini kilichofanyika leo Februari 13,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda, wakati akifungua Mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wenye lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye mazao hayo nchini kilichofanyika leo Februari 13,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda, akijadili jambo na Katibu Mkuu wake Bw.Gerald Kusaya,katika Mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wenye lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye mazao hayo nchini kilichofanyika leo Februari 13,2021 jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya,akizungumza katika Mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wenye lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye mazao hayo nchini kilichofanyika leo Februari 13,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James,akizungumza katika Mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wenye lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye mazao hayo nchini kilichofanyika leo Februari 13,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge,Mifugo,Kilimo na Maji Mhe. Christina Ishengoma,akizungumza katika Mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wenye lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye mazao hayo nchini klichofanyika leo Februari 13,2021 jijini Dodoma
Mwenyekiti wa TCCIA kutoka Mkoa wa Songwe Bw.Charles Chenza akitoa taarifa ya Mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wenye lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye mazao hayo nchini klichofanyika leo Februari 13,2021 jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki wakifatilia Mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wenye lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye mazao hayo nchini klichofanyika leo Februari 13,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wenye lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye mazao hayo nchini kilichofanyika leo Februari 13,2021 jijini Dodoma.
PICHA ZOTE NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
…………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma.
Waziri wa Kilimo Prof.Aldof Mkenda amefungua Mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wenye lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye mazao hayo huku akisema kuwa watahakikisha wanashirikiana na sekta binafsi ili kukuza kilimo nchini.
Mkutano huo umefanyika jijini Dodoma huku ukihudhuria na wafanyabiashara mbalimbali,Taasisi binafasi pamoja na baadhi ya viongozi kutoka wizara tofauti tofauti.
Prof.Mkenda amesema kuwa Sekta binafsi wamekuwa mstari wa mbele kuchangamkia fursa mara zote zinapoibuka ni kundi ambalo halihitaji kupigiwa mluzi wala kupokea maelekezo kutoka kwa viongozi.
Amesema kuwa changamoto ipo kwa watendaji serikalini ambao wakati mwingine wamekuwa wababaishaji na wacheleweshaji wa mambo, hata siku moja huwezi kuona sekta binafsi ikifanya ubabaishaji.
“Huwa najiuliza kwanini hatufanikiwi wakati watanzania sio wavivu, serikali tunajiuliza kuna tatizo gani, naamini mkutano wa leo utajadili suala hili na kutoa majibu ya msingi,”amesema Prof.Mkenda
Hata hivyo amesema kuwa fursa za kiuchumi zipo nyingi, masoko yakiwa imara watu watabuni mbinu ya kuzalisha na kuendelea kujiinua kiuchumi katika mazao ya biashara ya nafaka wanayofanya.
Aidha amelishukuru shirika la kilimo Afrika (AGRA) kwa kuandaa mkutano huo ambao utasaidia kuibua mambo muhimu ya msingi ambayo yatasaidia sekta hiyo na kuinuka zaidi uchui kwa kuliingizia pato taifa.
Kwa upande wake Katibu mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amewataka wadau kutumia fursa ya Mkutano huo kujadili na kueleza changamoto zinazowakabili ili Serikali iweze kuzishughulikia kwa maslahi mapana ya Taifa hasa katika suala la ukuaji wa uchumi wa nchi.