Kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC- TROIKA ) kilichofanyika kwa njia ya Mtandao kimeridhia mapendekezo ya Mawaziri wa Afya wa SADC kutaka kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC kifanyike kwa njia ya Mtandao ili kukabiliana na janga la ugonjwa wa COVID 19 katika ukanda wake.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha (Mb) aliyeshiriki kikao hicho cha SADC Troika akimuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kikao hicho kilikutana kwa ajili ya kupitia na kujadili mapendekezo ya Mawaziri wa afya wa SADC kilichofanyika Februari 29, 2021.
Amesema Mawaziri wa Afya walipendekeza kuwa kikao cha Baraza la Mawaziri kifanyike kwa njia ya mtandao na kikao cha Wakuu wa Nchi kilichokuwa kifanyike mwezi Machi kisogezwe mbele ambapo sasa kitafanyika kati ya mwezi Mei au Juni kutegemeana na hali ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19 itakavyokuwa na kuongeza kuwa vikao vingine vyote vitafanyika kwa njia ya mtandao hadi hapo hali ya maambukizi itakapokuwa imetengemaa.
Vikao hivyo viwili vilikuwa vifanyike mwezi Machi ana kwa ana nchini Msumbiji
Utatu wa SADC-TROIKA kwa sasa unaundwa na nchi za Msumbiji, Tanzania na Malawi umefanya lichofanyika kwa njia ya mtandao kulikutana kujadili taarifa ya kikao cha Mawaziri wa Afya wa SADC kilichokaa tarehe 29 Februari kuangalia hali ya ugonjwa wa COVID 19 katika ukanda wa SADC ambacho kiliamua kuwa kikao cha Baraza la Mawaziri kifanyike kwa njia ya Mtandao
Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha maafsa waandamizi ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge alishiriki kikao hicho ambacho pia kilifanyika kwa njia ya Mtandao.