Katibu mkuu wa wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Professa Mabula Mchembe akiongea na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutembea hosipitali ya ALMC Arusha.
katibu mkuu wa wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Profesa Mabula Mchembe akizungunza na baadhi ya watumishi wa hosipitali ya Maunt Meru alipokuwa katika ziara ya kushtukiza.
Kushoto ni katibu mkuu wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Profesa Mabula Mchembe akiongea na Mkurugenzi wa hosipitali ya ALMC Dkt Paul Kisanga
Kushoto ni katibu mkuu wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Profesa Mabula Mchembe akiongea na Mganga mfawidhi wa hosipitali ya Maunt Meru Dkt Alex Ernest
………………………………………………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Katibu mkuu wa wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Profesa Mabula Mchembe amewatoa wananchi hofu juu taarifa za uongo zinazosambaa kuwa hosipitali zimejaa wagonjwa na badala yake kuwataka kwenda kupata huduma kwani hali haipo kama inavyosemekana.
Profesa Mchembe aliyasema hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hosipitali ya Arusha Lutheran medical Center(ALMC) inayomilikiwa na kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini kati pamoja hosipitali ya rufaa ya Maunt Meru ili kujiridhisha kama ni kweli hakuna nafasi kama inavyozungumzwa katika mitandao ya kijamii.
Alisema kuwa amepata muda wa kupitia wagonjwa katika hosipitali ya ALMC yenye wa vitanda 160 ambapo ameona kuna wagonjwa waliolazwa kwa matatizo ya aina mbali ikiwemo figo, kupumua, upasuaji na mengineyo lakini kuna vitanda ambavyo havina watu na vipo tayari kwaajili ya kuhudumia wagonjwa.
“Nitoe rai kwa wananchi kwamba wanapopata changamoto ya kuumwa ni vema wakaenda mahosipitalini kusema wanajitibia majumbani kwani hosipitali zimejengwa kwaajili ya kuwahudumia lakini pia wajitahidi kupima afya zao kwasababu sio matatizo yote yanahusika na ugonjwa wa Corona, mengine pia yanahitaji matibabu na mfumo wa hewa ufanye kazi ila inategemea na hatua iliyofikia,” Alieleza Profesa Mchembe.
Aidha pia katika hosipitali Mount Meru ambayo ni hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha yenye uwezo wa kulaza watu 500 alisema kuwa ameona hali ilivyo na vitanda karibia 300 vina wagonjwa wa aina mbalimbali lakini ameona kuna changamoto ya wagonjwa kutolewa kwenye vituo vya afya na kwenda katika hosipitali hiyo kwa kuchelewa.
“Wananchi tujitahidi kufika hosipitali mapema ili tuweze kupata huduma nzuri na inayostahili kwani hakuna hofu kubwa kama inavyosemekana kuwa kuna ugonjwa ambao unatishia maisha ya watu,” Alisema.
Pia alisema kuwa wizara imeagiza baadhi ya mifumo ya kutengenezea oksijen ambayo watazielekeza katika hositali saba za rufaa za mikoa kwani walikuwa wanategemea sana mitungi ambapo wakiwa na mifumo hiyo wataweza kuboresha huduma zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa hosipitali ya ALMC Dkt Paul Kisanga alisema kuwa changamto inayokabili katika kupokea wagonjwa wa aina mbalimbali ni watu kwenda wakiwa wamechelewa na sio tu kwa matatizo ya kifua bali hata wa magonjwa mengine kutokana na kuanza kujitibu nyumbani.
“Watu wakija mapema inatupa nafasi ya sisi kuwatibu mapema na matokeo yakawa mazuri zaidi na kuweza kuwarudisha katika mzunguko wa kulijenga taifa lakini wanapokuja kwa kuchelewa matokeo yake yanakuwa sio mazuri na pia inakuwa ni ghali sana,”Alisema
Alieleza kuwa kama mtu anajisikia vibaya mahali pa kwenda ni hosipitali wawaache wataalamu wafanye kazi, wawaone na kuwashauri na sio kubaki na dhana ya kuwa hosipitali kumejaa alafu baadae wanaenda wakati hali ikiwa mbaya.
Naye Mganga mfawidhi wa hosipitali ya Maunt Meru Dkt Alex Ernest alisema kuwa hosipitali hiyo ipo kwaajili ya kuwahudumia wananchi wote wenye magonjwa ya aina mbalimbali hivyo mwananchi yoyote anapokuwa na tatizo la kiafya anapaswa kuwahi hosipitali ili aweze kupata huduma inayostahili na kwa wakati ambapo wana oksijeni za kutosha, wahudumu, pamoja na kuweza kutoa huduma zote.