Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akizungumza na Wafugaji (hawapo pichani) katika kikao cha kujadili Maendeleo ya Sekta ya Mifugo kilichofanyika jijiji Dodoma Februari 10, 2021.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro walipokutana katika kikao cha kujadili Maendeleo ya Sekta ya Mifugo kilichofanyika jijini Dodoma Februari 10, 2021.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya wafugaji waliohudhuria kikao cha kujadili Maendeleo ya Sekta ya Mifugo kilichofanyika jijiji Dodoma Februari 10, 2021.
Mmoja wa Wafugaji kutoka Wilayani Kilindi, Mkoani Tanga, Yohana Samwel akieleza jambo katika kikao cha kujadili Maendeleo ya Sekta ya Mifugo kilichofanyika jijiji Dodoma Februari 10, 2021.
Mkurugenzi, Idara ya Uendelezaji Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Dkt. Asimwe Rwiguza (kulia) akisikiliza hotuba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili Maendeleo ya Sekta ya Mifugo kilichofanyika Februari 10, 2021. Kushoto ni Katibu wa Chama cha Wafugaji, Joshua Lugaso.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro walipokutana katika kikao cha kujadili Maendeleo ya Sekta ya Mifugo kilichofanyika jijini Dodoma Februari 10, 2021.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akifurahia jambo na Mmoja wa Watumishi wa Mwanzo wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Mzee Mosses Mpeku (Mstaafu) walipokutana katika kikao cha Chama cha Wafugaji kujadili Maendeleo ya Sekta ya Mifugo kilichofanyika jijini Dodoma Februari 10, 2021.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akiwa katika picha ya pamoja na Wafugaji mara baada ya kikao cha kujadili Maendeleo ya Sekta ya Mifugo kilichofanyika jijiji Dodoma Februari 10, 2021.
…………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imeiagiza Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kuwanyang’anya wale wote walioshindwa kuendeleza vitalu walivyokodishwa kwa sababu wamekiuka masharti ya mkataba.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mhe.Mashimba Ndaki,wakati wa kikao na Viongozi wa Chama cha Wafugaji katika kikao cha kujadili Maendeleo ya Sekta ya Mifugo kilichofanyika jijiji Dodoma Februari 10, 2021.
Mhe.Ndaki amesema kuwa kuna watu wengi wamekodishwa maeneo katika ranchi za taifa lakini wamezitelekeza na wengine wamekodisha watu wengine ambao wanatumia maeneo hayo kinyume na makubaliano ya mkataba.
“Ikifika tarehe 15 mwezi huu, wale wote waliochukua vitalu na wamekodisha watu wengine wanyang’anywe maeneo hayo na hatutajali mikataba yao kwani wameshakiuka masharti,” amesema Ndaki
Aidha Mhe.Ndaki amesema kuwa baada ya tarehe 15 kupita wataanza kuwasaka wote waliochukua maeneo hayo na kuwanyang’anya ili wapewe wafugaji makini waweze kutumia maeneo hayo kuweka mifugo yao.
Kuhusu baadhi ya Wananchi wanaoishi karibu na ranchi kuvamia maeneo hayo, Ndaki alitumia nafasi hiyo pia kuwataka waondoke katika maeneo hayo na wasipofanya hivyo wataondolewa.
Hata hivyo amesema kuwa wameanza mikakati ya kuiweka vizuri NARCO ili maeneo makubwa iliyonayo ambayo mengine hawayatumii vizuri yagawiwe kwa wafugaji watakaoweza kuyatumia kufanya ufugaji wa kisasa nah atua waliyoanza nayo ni kupunguza bei ya kukodisha vitalu.
“Tumekubaliana kuwa bei ya kukodisha kitalu iwe ni shilingi elfu tatu mia tano (3500) kwa Ekari moja na sio zaidi ya hapo,” amesema Ndaki
Mhe.Ndaki amesema kuwa wameielekeza NARCO kuwa katika yale maeneo waliyoyatenga kwa ajili ya ukodishaji watenge asilimia thelathini (30) kwa ajili ya kuwakodisha wafugaji wanaoishi karibu na maeneo ya ranchi hizo ili kupunguza migogoro na uvamizi wa maeneo hayo.
“Hata maeneo yetu yaliyotengwa kwa ajili ya kupumzishia mifugo (holding grounds) tutayapunguza ili nayo tuwape NARCO ili wayakodishe kwa wafugaji wetu, tunaamua kufanya haya ili kutibu tatizo la malisho na wafugaji waondokane na kutangatanga,” amesisitiza Ndaki
Mapema wiki hii Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NARCO, Paul Kimiti alitangaza kuwa ekari moja ya kitalu katika ranchi hizo itakodishwa kwa shilingi elfu tatu mia tano (3500).