Ni wakulima wakipata maelezo ya matumizi ya dawa ya viuagugu kwenye mpunga
………………………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Kampuni ya usambazaji wa pembejeo za kilimo (Mams) imetatua changamoto ya wakulima nchini wa zao la mpunga ,kufanya palizi kwa kutumia jembe la mkono kwa kuleta viuagugu mathubuti vya kupalilia zao hilo .
Akiongea na waandishi wa habari afisa masoko wa kampuni hiyo Julias Nambua alisema kuwa wamefanya utafiti wa kina na kuona kuwa ni viambato amilifu vya aina gani vingeweza kutatua tatizo sugu la magugu kwenye zao la mpunga .
” kiuwagugu hicho tulichokisajili ni multrice plus 250D yenye viambato amilifu viwili ndani yake na multrice extra 300D chenye viambato amilifu vitatu ndani yake “alisema Nambua
Aidha alisema kuwa viuagugu hivyo wigo mpana wa kuangamiza magugu yote magumu yanao wasumbua wakulima wa zao la mpunga Kama vile ndago,sangari,salad,punga pori pamoja na Mwenyekiti ambapo dawa hizi zitafanya wakulima kulima kwa tija.
“kwa kutumia dawa hizi mmea wa mpunga utapa virutubisho ama lishe sahihi kutoka arithini pasipo ushindani wa magugu kwani bei zake ninafuu sana kwa mkulima ,”Alisema Nambua.
Alifafanua kuwa dawa hizo zitawafanya wakulima kulima kwa tija kwani mmea wa mpunga utapata virutibisho ama lishe sahihi kutoka kwenye udongo na kulisha mmea kuliko kuwa shindani kati ya magugu na mpunga hivyo
kupelekea mpunga kustawi vizuri na kuzalisha mazao mengi na yenye bora.
Aidha Nambua alisema Mams Limited imeagiza buti maalumu zitakazotumiawa na
wakulima wa mpunga ambazo ni nyepesi na zitamkinga mkulima na mpulizaji wa dawa dhidi ya kemilaki za dawa na wadudu wanaongata na kusababisha madhara katika mwili Kama vile kupata magonjwa Kama kichocho yanayotokana na maji ya mpunga yaliyotwama kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtengaji wa kampuni hiyo William Mbaruk alisema dawa hizo ni neema na ukombozi kwa wakulima wa hapa nchini kwani wakizitumia vyema wataweza kufanya mapinduzi ya kweli ya kilimo kwenye uzalishaji wa zao la mpunga.
Alisema lengo la kampuni hiyo ni kumpatia
mkulima pembejeo zilizo bora na kwa bei nafuu na kuwapatia elimu kupitia mashamba darasa wakishirikiana na maafisa ugani
“Dawa hizi za palizi ya mpunga zinasambazwa kote nchini kupitia TFA ambaye ni wakala
mkubwa wa Mams limited na wana matawi mengi hapa nchini na ni taasisi kogwe ya mapinduzi ya kijani hapa nchini na pia zinapatikana kwa mawakala wa pembejeo,” Alisema Mbaruk.
Sambamba na hayo alitoa wito kwa waliohitimu vyuo mbalimabali kujihusisha na kilimo cha mpunga kwani kinalipa na ni ajira
kwao kuliko kukaa na kusubiria ajira serikalini hasa wakati huu ambapo serikali imeweka
sera nzuri za maedeleo ya nchi katika uzalishaji wa mazao ya kilimo biashara.
Alisema kwa kufanya kilimo kwa kutumia technologia za kisasa zenye tija ambazo hazimchoshi mkulima na kumwezesha kulima mashamba makubwa tofauti na awali ambapo walikuwa wakisumbuliwa na magugu na magojwa ya njano kwenye zao la mpunga ambazo kwa sasa ufumbuzi umepatikana.
Hata hivyo zao la Mpunga ni kati ya mazao maarufu hapa nchini kwa uzalishaji kwa ajili ya chakula na biashara na huzalishwa maeneo yanayotwaa maji ambapo huzalishwa katika majoruba kwani huhitaji maji mengi wakati wa uzalishaji na uzalishaji wa zao hili huchangia pato la Taifa na hutoa ajira nyingi
Meneja masoko wa Mams Julius Nambua akiendelea kutoa elimu juu ya madawa ya mpunga kwa wakulima wa zao la mpunga.