…………………………………………………………………………………
NJOMBE
Wakati soko la zao la parachichi likizidi kufunguka kimataifa ,wakulima wa zao hilo mkoani Njombe wameomba serikali na wadau wengine wa kilimo kuwasaidia kuboresha miundombinu ya barabara zinazoelekea maeneo ya uwekezaji ili mazao hayo yasipoteze viwango vya ubora wa kimataifa wakati wa usafirishaji.
Mbali na changamoto ya barabara wakulima hao wamezitaja changamoto nyingine zinazokwamisha jitihada za kufanya kilimo bora na chenye tija sokoni kuwa ni majanga ya asili ya ukungu,barafu na uhaba wa maji .
Frank Msuya,Hery Nyagawa na Teresia Nyato ni baadhi ya wakulima waliowekeza ekari zaidi katika kilimo hicho ambapo wanaeleza namna zao la parachichi linavyokwamishwa na miundombinu mibovu ya barabara zinazoelekea mashambani na kisha kuelekeza ombi lao serikalini na taasisi ma wadau wengine wa kilimo.
Licha ya changamoto hizo lakini bado mamia ya wakulima kutoka mikoa mbalimbali wamekuwa wakimiminika mkoani Njombe kujifunza kwa vitendo kilimo hicho huku wakidai sababu kubwa ni uhakika wa soko lake ambalo limekuwa likikua kila uchwao Kama ambavyo Geofrey Ngogo Katibu mkuu wa KKKT dayosisi ya Kusini Magharibi
Awali akitoa elimu ya kilimo cha parachichi mkufunzi wa kilimo hicho shambani kwake Obed Mgaya amesema licha ya mkoa wa Njombe kuhamasika lakini wakulima waengi wanapanda zao hilo na kushindwa kuhudumia jambo ambalo linawafanya kushindwa kupata mazao yenye ushindani sokoni.
Bei ya zao laparachichi inazidi kupaa kutoka elfu 1500 mwaka jana hadi 1800 mwaka huu jambo linalovutia wengi kuwekeza.