wanafunzi wa darasa la kwanza wakiwa darasani katika moja ya shule za msingi katika manispaa ya Mpanda
Meya wa Manispaa ya Mpanda Haydari Sumri akiendesha kikao cha baraza la Madiwani
……………………………………………………………………………
Na Zillipa Joseph, Katavi
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imeandikisha jumla ya wanafunzi 3931 wa darasa la awali kwa mwaka 2021 sawa na asilimia 75 ya makisio ya uandikishaji kwa mwaka huu
Akitoa taarifa kwa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Mpanda Afisa Elimu Msingi Josephat Kalulu amesema wavulana ni 1925 na wasichana 2056 na makisio yalikuwa kuandikisha wanafunzi 5311
Aidha kwa upande wa darasa la kwanza wameandikisha wanafunzi 6392 ambapo wavulana ni 3221 na wasichana ni 3171 sawa na asilimia 77; ambapo makisio ya uandikishaji yalikuwa ni wanafunzi 8317
Alieleza kuwa hata hivyo bado wanendelea kupokea wanafunzi kwani zoezi la uandikishaji bado halijafungwa mpaka katikati ya mwezi wa tatu
Kwa upande wa shule za sekondari asilimia 86 ya wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza; wameripoti katika shule walizopangiwa
Bi. Leticia Lutunguru ni Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Mpanda alisema wanafunzi 2599 wameripoti katika shule mbalimbali walizopangiwa ambapo wavulana ni 3101 na wasichana ni 1298
Aliongeza kuwa ni asilimia 14 tu ya wanafunzi ambao bado hawajaripoti
Naye Meya wa Manispaa ya Mpanda Haydari Sumri amesema Halmashauri imebadilisha matumizi ya fedha shilingi milioni mia moja zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa gari la meya na kupeleka katika kutatua changamoto katika shule mabalimbali
Sumri ameeleza kuwa shilingi milioni sabini zitaelekezwa kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa na shilingi milioni thelathini zitatengenezewa madawati