Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (Aliyesimama) akifungua Kikao cha kupitia, kujadili na kupitisha Katiba ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Fungu 51). Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mkutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Emmanuel
Kayuni (Wakwanza kulia) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (Katikati) pamoja na Watumishi wa
Wizara hiyo (Hawapo pichani) katika Kikao cha kupitia, kujadili na kupitisha Katiba
ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Fungu
51). Wakwanza kushoto ni Mjumbe wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo, Bi. Sabina
Ntonda, ambaye amewakilisha Uongozi wa chama hicho. Kikao hicho kimefanyika
katika Ukumbi wa Mkutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio
(Wakwanza aliyevaa miwani) akiwasili katika Ukumbi wa Mkutano wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji ambapo alifungua Kikao cha kupitia, kujadili na kupitisha
Katiba ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
(Fungu 51). Kikao hicho kimefanyika Jijini Dodoma leo Februari 08, 2021.
Mkaguzi wa Zimamoto, Rehema Menda (Aliyesimama) akifafanua jambo kuhusiana na Mfuko wa Faraja wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (Hayupo pichani), baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo na Watumishi waliohudhuria Kikao cha kupitia, kujadili na kupitisha Katiba ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Fungu 51).
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Christopher kadio (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na Watumishi hao katika Kikao cha kupitia, kujadili na kupitisha Katiba ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Fungu 51). Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dodoma Februari 08, 2021.