……………………………………………………………………………..
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MKUU wa wilaya ya Kibaha ,mkoani Pwani ,mhandisi Martin Ntemo, ametoa siku mbili kwa wafanyabiashara ndogondogo wa Soko la Picha ya Ndege ,kuondoka katika eneo la hifadhi ya barabara ili kumpisha mkandarasi aendelee na ujenzi wa barabara kuu .
Akizungumza na wafanyabiashara hao a,katika soko hilo ,alieleza amesikia malalamiko kuwa kuna baadhi ya wafanyabishara wanadaiwa kuchochea kuwashinikiza wafanyabiashara wengine wasihame katika eneo lililotengwa.
Ntemo alisema wafanyabiashara walitakiwa kuhamia , eneo la shirika la elimu ambalo lipo river road Msufini lakini walikaidi na kudai kuwa hakuna huduma muhimu kama vile umeme, na sio eneo la kudumu.
“Hili eneo ni hatarishi na Tanroad walishawaelekeza wahame ili mkandarasi aendelee na ujenzi , ikanisukuma nikaenda kuzungumza na taasisi ya shirika la elimu wakaruhusiwa waendele na biashara zao lakini nikabaini kuna wafanyabiashara wachochezi wanaoshawishi wenzao Wagome kuhamia katika eneo hilo”
Msimamizi wa mradi huo kutoka TANROADS
Charles Rwetabura, alifafanua wafanyabishara hao wanapaswa kuondoka kwenye eneo la mradi wa kuboresha maeneo hatarishi kwa malengo mawili ikiwemo
Sheria ya barabara namba 13 ya mwaka 2007, inayowataka wananchi waliovamia maeneo hatarishi waondoke , lakini pia suala la usalama.
Diwani wa kata Sofu ,Musa Ndomba alisisitiza wajasiriamali hao , kutii agizo hilo na kuhama ambapo kwasasa itakuwa eneo la kudumu ili kuleta maendeleo na kuinua uchumi wa kata hiyo.
Awali mmoja wa wafanyabishara hao ,Daniel Singa alibainisha mgogoro huo ni wa takriban miaka sita ambapo mwanzo walitakiwa kuhamia eneo la Lulanzi ambako waliona ni mbali , baadae wakatakiwa kuhamia eneo la River road ambako wachache waligomea .
Singa alielezea kwamba ,kwa sasa wametii agizo la serikali na wataondoka kwa ajili ya maendeleo yao.