Mchungaji wa Power of God Fire Church, Dankton Rweikila.
*****************************
WATANZANIA wametakiwa kupuuza taarifa za uzushi zinazotolewa na wapotoshaji na badala yake waamini na kulishikilia neno la Mungu kwenye changamoto zote ikiwamo ya janga la covid-19.
Wito huo ulitolewa na Mchungaji, Dankton Rweikila, kutoka Kanisa la Power of God fire Church jijini Dar es Salaam na kusisitiza umuhimu wa kumuamini Mungu katika majanga yote yatakayolikumba taifa.
“Kabla haujamuamini Mungu yeye anakuaminisha kuwa ana nguvu ndiyo maana huwezi kumuamini bali kazi anazozifanya zitakuaminisha kuwa yeye ni nani. Kitu kinachofanyika pale unapomdharau mtu huku ukijua uwezo wake anaona ni dharau hivyo anachukia ni kwa sababu unajua uwezo wake unamjua Mungu wa Tanzania.
“Akitokea mtu ambaye amuamini Mungu kwa maana hajajifunua kwao hiyo ni sawa lakini sisi Tanzania tunayo sababu ya kuamini, ndiyo maana hatushangai mataifa mengine yakitushangaa kwa sababu hawamjui Mungu wa Tanzania ndiyo maana hawana uwezo wa kupambanua kati ya Mungu mwenye nguvu na taifa lenye nguvu,” alisema.
Mchungaji Rweikila alisema Tanzania haina budi kumuheshimu na kumthamini Mungu kwani ndiye aliyelisaidia taifa kupambana na majanga mbalimbali.
Aliongeza kuwa kinachoshuhudiwa kwa baadhi ya watu wanaoheshimu mataifa mengine badala ya Mungu ni ishara kwamba utegemezi wao upo kwa mataifa hayo.
“Unaweza kusema bahari inaweza kugawanyika lakini mataifa yenye nguvu hapana! Naongelea habari za Mungu aliyewapigania wana wa Israeli na mataifa makubwa sana (Hesabu 31:8) walikuwa hawana jeshi lakini aliwashindia,” alisema.
Kwa mujibu wa Mchungaji huyo, suala la Tanzania kufungiwa mipaka na baadhi ya mataifa ni jambo la kawaida kwakuwa msingi wa ukombozi wa Tanzania ni Mungu muweza wa yote.
Alisema neema ya Mungu iliyopo Tanznaia ndiyo imeliepusha taifa na magonjwa mbalimbali ikiwamo Malaria na mengine.
“Mfumo wa dunia ulisema hivi covid-19, ilipoingia kwamba tuvae barakoa na sanitizer, vitu kama hivyo tukavua na kusema hii haijazoeleka kwenye vita Daudi akasema nipe mawe matano na jiwe kisha akamuendea Goliath,” alisema.
Mchungaji Rweikila alisema nu muhimu kumshukuru Mungu kutokana na kuendelea kwa shughuli mbalimbali nchini wakati hali ni tofauti kwa mataifa mengine.
“Wao wanakwenda Bungeni kuitisha bajeti ya Corona lakini sisi tunapanga bajeti ya barabara, maji, umeme, madarasa wanauliza nyie vipi mbona hakuna ya Corona, tusimdharau Mungu Watanzania.
“Usimdharau Bwana, viongozi, Mawaziri, Wabunge , Wakuu wa Mikoa , Wachungaji, Maaskofu, Manabii, Mitume, Waijilisti tusiogope yupo Bwana aliyetuokoa mwaka jana” alisema.