Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Ranchi za Taifa Limited (NARCO) Paul Kimiti akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati mbalimbali za Ranchi nchini Jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa NARCO Emmanuel Mnzava akizungumza kuhusiana na taratibu za mtu kufanya uwekezaji wa ufugaji katika Ranchi zilizopo nchini.
***********************************************
*Ni kuhusiana na Tozo Moja kutoa katika mikataba ya uwekezaji
Kampuni ya Ranchi za Taifa Limited (NARCO) limesema kuwa kuanzia sasa limeweka tozo moja ya sh.3500 kwa ekari ndani ya mwaka kwa mikataba mipya ya upangishaji wa vitalu kwa ajili ya kufanya ufugaji wa kibiaashara na Kisasa.
Tozo hizo hazitahusu wale wenye mikataba ya zamani ni mpaka pale wataporekebisha mikataba yao na kuanza kulipa tozo hizo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi wa Kampuni Paul Kimiti amesema kuwa kuweka Tozo moja ni agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwa mkoani Kagera alipotembelea Mmoja ya mwekezaji moja ya Ranchi mkoani humo.
Amesema licha ya kuweka Tozo amewataka wananchi wawekeze katika ufugaji wa Ranchi kwani maeneo mengi na hayana kugombania malisho kutokana utaratibu ulivyowekwa wa kuwa na malisho ya Kisasa.
Amesema wawekezaji waliopo ni zaidi ya 200 ambao hata robo ya ardhi ya ranchi haijafikia katika eneo hilo.
Amesema tozo hizo ya mikataba mipya ya uwekezaji itahusisha Ranchi 14 zilizopo katika Mikoa Tisa ya Tanzania Bara ambazo ni Kongwa iliyopo Dodoma,Ruvu mkoani Pwani, Mkata ,,Dakawa Morogoro,Kalambo Rukwa,West Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro, Mzeri Hill Tanga,Missenyi,Kitengule mkoani Kigoma,Mabale na Kikulula mkoani Kagera,Uvinza Kigoma, Usangu Mbeya zote zikiwa na jumla ya hekta 627,164.
Nae Meneja wa Masoko wa NARCO Emmanuel Mnzava amesema kuwa uwekezaji huo watu wenye Ng’ombe wawili wanaweza kuunda kikundi na kupata Ranchi kwa ajili ya kufanya ufugaji wa kibiaashara na kisasa.
Amesema milango ipo wazi kwa watanzania kuwekeza katika ufugaji kwani ardhi ni kubwa.
Amesema ufugaji wa kisasa ni ule Ng’ombe akiwa na umri mdogo kuwa na kilo nyingi.