…………………………………………………………………….
Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) umetangaza kutoa ruzuku ya Shilingi milioni 5 kwa kila andiko la mradi inayohusiana moja kwa moja na upandaji miti katika shule za msingi na sekondari kutoka wilaya 18 za mikoa nane ya nyanda kame.
Hayo yamebainishwa hii leo na Afisa Miradi wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) Juma Ally wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya nne ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayoendelea katika Uwanja wa Sheikh Amri Abed Arusha
“kwa mjibu wa Tangazo lililotolewa TaFF la uhitishaj wa maandiko ya miradi kuwa kipaumbele cha utoaji wa ruzuku hiyo kitakuwa ni pamoja na miradi inayohusiana moja kwa moja na upandaji miti katika nyanda kame itakayohushisha Shule za misingi na Sekondari”amesema Ally,
Amesema mwisho wa kupokea maandiko ya miradi inayoomba ruzuku ndogo ambazo shule hizo zinapaswa kuomba ni Juni 30, 2021 kwa awamu ya kwanza na Desemba 31, 2021 awamu ya pili.
Pia amesema ruzuku ndogo isiyozidi Shilingi milioni 5 itatolewa kwa shule za msingi na sekondari kutoka wilaya 18 na mikoa nane ya nyanda kame kama vile Dodoma Wilaya za Dodoma ni Chamwino,Mkoa wa Singida Wilaya zake ni Ikungi,Mkoa Shinyanga Wilaya yake ni Kishapu,Mkoa wa Simiyu Bariadi na Busega,
Ameongeza Mkoa wa Manyara Wilaya zake ni Babati na Hanang,Mkoa wa Arusha Wilaya zake ni Arumeru,Monduli na Longidoo,Mkoa wa Kilimanjaro maeneo ya tambarare na Wilaya za Rombo na Same,Mkoa wa Kagera Wilaya zake ni Biharamulo,Karagwe ppamoja na Ngara
“Ili shule ipate ruzuku hiyo inapaswa kutimiza vigezo vyote vya maandiko ya miradi vinavyotumika wakati wa kuchagua miradi itakayopatiwa ruzuku na mfuko” amesema Ally
Hata hivyo aliongeza kuwa Shule hizi kabla ya kuomba ruzuku hizo zinapaswa kupata ruksa kutoka kwa wakurungezi wa halmashauri husika pia, ushauri wa wataalam wa misitu pamoja na kuwa na maeneo kwa ajili ya uanzishwaji wa vitalu vya miti shuleni na upandaji wa miti.
“Shule zitakazofanikiwa kupatiwa ruzuku zinategemewa kutoa hamasa ya upandaji miti katika shule na vijiji vya jirani,” ilisema taarifa hiyo. Mbali ya shule hizo za Nyanda Kame, Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) unahitisha maandiko ya miradi kutoka kwa vikundi vya kijamii, asasi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na uhifadhi, usimamizi na uendelezaji wa rasilimali misitu.
Ufugaji nyuki ni ajira mbadala inayochangia kupunguza uharibifu wa misitu na kuongeza mchango wa sekta ya maliasili katika pato la Taifa. Kutokana na umuhimu huo Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF), umepanga kutoa ruzuku kwa vikundi vya wanawake na vijana katika miradi ya ufugaji nyuki inayolenga uhifadhi wa misitu ya asili katika Mikoa ya Lindi, Mbeya, Songwe, Rukwa, Tabora, Shinyanga, Kigoma na Katavi. “Kipaumbele katika miradi hii watapewa vikundi vya wanawake na vijana wanaojihusisha na ufugaji nyuki,
Pia watapatiwa mafunzo ya kutengeneza mizinga bora ya nyuki.” Vikundi hivi pia vinaweza kupatiwa ruzuku ya fedha kwa ajili ya kugharimia utekelezaji wa shughuli zilizoainishwa kwenye maandiko yao ya miradi.