Mhifadhi
mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita akiwa katika akishuhudia tukio la afisa tawala ofisi ya
mkuu wa wilaya ya Mufindi,Joseph Mchina akikabidhi miche ya miti kwa kiongozi wa kikosi cha JKT Mafinga
Na Fredy Mgunda,Iringa.
ZAIDI ya miche ya miti milioni moja yenye gharama ya shilingi milioni
200 hugawiwa kwa wadau na wananchi mbalimbali wa wilaya ya Mufindi kwa lengo la
kuendelea kuboresha mazingira ya misitu na kutunza uoto wa asali na wakala wa
huduma za misitu Tanzania TFS kupitia shamba la miti la Sao hill Mkoani Iringa.
Akizungumza wakati kugawa miche hiyo kwa wananchi na wadau mbalimbli,Mhifadhi
mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita alisema lengo la kutoa
miche hiyo kuendelea kuchukua hatua madhubuti za ulinzi shirikishi wa misitu na
uhifadhi wa mazingira ili kuondosha hatari zitokanazo na uharibifu wa mazingira
Alisema kuwa Jamii,Taasisi mbalimbali na mashirika ya Umma
yamesisitizwa kuendelea kuthamini na kutunza mazingira kutokana na umuhimu wake
kwenye maisha ya binadamu.
Alisema ni jukumu la kila mmoja kuendelea kuyatunza mazingira na hasa juu ya
ulinzi wa Bayoanuai zilizopo ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa viumbe hai
wote wakiwamo Binaadam huku
akitaja za kutoweka kwa bayoanuai
Mwita alieleza namna ambavyo Shamba la Miti Sao Hill linavyohamasisha jamii
kuendelea kuyatunza mazingira kwa kuihusisha katika shughuli rafiki za uhifadhi
wa masitu ikiwamo ajira na ufugaji wa nyuki.
Alisema kuwa misiti imekuwa na faida mbalimbali kwa viumbe vyote duniani
ikiwepo kuwa makazi ya wadudu,wanyama,ndege na eneo sahihi kujipatia
chakula,ikolojia ya misitu ya Sao Hill imechangia sana upatikanaji wa maji ya
mto Ruaha Mkuu na Ruaha Mdogo ambavyo hupeleka maji katika vituo vya kuzalishia
umeme.
“Umeme unazalishwa katika vituo vya Mtera,Kihansi na mwalimu Nyerere
wanategemea maji kutoka katoka hidhafi ya misitu ya Sao Hill kutokana na
utunzaji bora wa ikolojia yake”alisema
Alisema upandaji wa miti unasaidia upatikanaji wa dawa mbalimbali za asili
ambazo zimekuwa zinasaidia katika maisha ya binadam hivyo misiti inaumuhimu
mkubwa sana kwa wananchi kote ulimwenguni.
Aidha Mwita alisema kuwa shamba la miti la Sao Hill limekuwa lanachangia kukuza
uchumi katika sekta mbalimbali kama viwanda,miundombinu na sekta ya ujenzi.
Akizungumza kwa niaba mkuu wa wilaya ya Mufindi,afisa tawala ofisi ya
mkuu wa wilaya ya Mufindi,Joseph Mchina alisema kuwa kitendo cha viongozi wa
shamba la Sao Hill kutoa miche ya miti milioni moja bure kwa wananchi wa wilaya
hiyo ni kukuza uchumi kwa wananchi wa wilaya ya Mufindi na Tanzania kwa ujumla
kutokana na faida za miti.
Alisema kuwa uwepo wa shamba la miti katika shamba hilo la serikali
limechangia kwa kiasi kikubwa kuwashawishi wananchi wengine wa wilaya hiyo
kuanza kupanda miti na hadi hii leo bado wanapanda miti na umekuwa uchumi wa
wananchi.
Mchina alisema kuwa kitendo cha kutoa miti hilo bure kunawakumbusha
wananchi kuendelea kupanda miti kwenye mashamba yao ili kuendeleza utamaduni wa
kupanda miti ili kukuza uchumi kwa wananchi wanaolizunguka samba hilo.
Aliwaomba wananchi wa wilaya ya
Mufindi kuacha tabia ya kukata miti hovyo ili kuokoa mazingira ambayo ndio
yamekuwa yanasababisha wananchi wanapata chakula,maji na kadharika hivyo
wananchi wanapaswa kupanda miti kwa wingi kwa lengo la kutunza mazingira.
“Ni vema tukaendelea kutunza miti ya asili na kuendelea kupanda miti
kwa kitaalamu kwa kufuata maelezo kutoka kwa wataalam ili kupunguza uharibu
unaosababishwa na sisi wenyewe kwani misitu ni mali na uhai vile vile” alisema
Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuendelea kupanda miti na kuitunza ili
kulinda mazingira na kukuza uchumi kwa wananchi na amewapongeza viongozi wa
shamba la miti la Sao Hill kwa jitihada za kuendelea kutunza mazingira.
Nao wadau wa mazingira kutoka Shamba la Miti Sao hill wameeleza namna wanavyonukaika
na uwepo wa shamba hilo la Serikali huku wakipongeza hatua zinazochukuliwa hasa
juu ya ulinzi wa mazingira.