*****************************************
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Viwanda Mhandisi Ramson Mwilangali akitoa hotuba ya ufunguzi katika Mashindano ya KAIZEN ambapo washiriki wenye Viwanda na wafanyabiashara watashindanishwa na washindi watatangazwa siku ya kilele cha maadhimisho ya KAIZEN tar 5 Februari, 2021 katika ukumbi wa LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Aidha washindi watakaopatikana leo watashiriki Mashindano ya KAIZEN kwa Africa nzima yanayotarjiwa kufanyika mwezi Juni 2021 nchini Tanzania.
Mashindano haya ya KAIZEN yanafanyika leo tar. 4 Februari, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa Dar es salaam ambapo wenye Viwanda wanawasilisha jinsi walivyotekeleza falsafa ya KAIZEN katika maeneo yao ya kazi.