*****************************************
NA NAMNYAK KIVUYO , ARUSHA
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo amegawa bima za afya za mfuko wa jamii NHIF 100 kwa watoto wenye ulemavu kutoka Kata zite 25 za jiji la Arusha.
Akiongea wakati wa kukabidhi bima hizo za afya mbunge huyo alisema kuwa utoji wa bima hizo ni mwendelezo utekelezaji wa ahadi zake alizozitoa kwa walemavu katika kampeni za uchaguzi 2020 ambapo alishatoa viti nwendo 10) kwa wakemavu 100.
Alisema kuwa lengo la kutoa bima hizo ni kuweza kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum kupata huduma ya afya uhakika katika vituo mbalimbali vya afya vilivyopo hapa nchinia mm ambapo ana lengo la kuwafikia walemavu wote 565 walopo jiji la Arusha.
Alibainisha kuwa huu sio mwisho wa kusaidia watoto na kufafanua kuwa bima hizi zitakapo isha ata changia tena kwa mwaka mingine,au wananchi ataendelea kuwasaidia kea kadri awezavyo kwani waliweza kumuamini na kumtuma akawaeakileshe bungeni na kuwapelekea kero zao ili ziweze kutatuliwa
Alieleza pia amesikia mzazi mmoja analalamika kuwa kuna baadhi ya shule zimekuwa zikikataa kuwapokea na kuwandikisha watoto wenye ulemavu na kuwaambia wazazi wawapeleke watoto kwenye shule zenye utindio wa ubongo wakati mtoto huyo akiwa anasumbuliwa na tatizo la miguu.
“Mimi ni seme tu swala hili nilikuwa sujalipata ndio nimelipata Ila niwaaidi nitalifanyia kazi,nitalifikisha kwa viongozi wenzangu akiwemo mkurugenzi wa halmashauri ,madiwani pamoja na mkuu wa wilaya Ili tuone ni namna gani tunaweza kutatua sala hili kwani ni haki ya kila mtoto kupata elimu”alisema Gambo .
Kwa upande wake mmoja ya mzazi aliepata msaada huu Asha Ally alimshukuru Sana mbunge kwa kuwajali watoto wao na kusema kuwa awali walikuwa wanateseka Sana haswa pale mtoto akiumwa na unakuta mzazi ana fedha za kumpeleka mtoto hospital hivyo bima hizo zitawasaidia Sana.
Zainabu aliomba serikali isaidie shule zenye watoto wenye ulemavu kuwajengea mazingira rafiki ya miundombinu Kama vyoo ,madarasa yao ambayo wataweza kunihudumia wenyewe pamoja na njia zao,ambapo pia aliongeza kuwa serikali iwadaidie kuwaelimisha walimu kuwa pokea watoto wenye ulemavu haswa wale wenye ulemavu wa viungo Kama miguu kwani nao wanawajibu wa kujipatia elimu
Nae mganga mkuu wa jiji la Arusha Dr.Kheri Kagya alisema kuwa jiji la Arusha Kuna watu zaidi ya 500 wenye ulemavu wa aina mbalimbali,wao Kama jiji wapo kwenye mkakati wa Kuhakikisha watu hao wanapata huduma staiki ambapo alisema kuwa wanampango wa kuwaita walemavu wote na kuwapa elimu ya Mkopo na ikiwezekana waanze kuwapa mikopo