***********************************
Katibu tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amefariki dunia Leo tarehe 3/2/2021 akipatiwa matibabu katika kituo Cha Afya Cha Magugu baada ya kupata ajali ya gari akielekea Dodoma Kikazi
Akitoa taarifa ya kifo hicho mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta amesema kuwa Ajali hiyo imetokea maeneo ya mdori baada ya gari lake kugongana uso kwa uso na basi la abiria la makara lililokuwa linatokea babati kuelekea Arusha.
“Baada ya hapo walimsaidia kumpeleka katika kituo Cha Afya Cha Magugu ili baadae wampeleke babati kwa matibabu zaidi lakini juhudi za.madaktari ndugu yetu Richard Kwitega akafariki saa Tisa na dakika 50″alisema Kimanta
Kimanta amesema kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara, Katibu tawala wa mkoa wa Manyara,pamoja na mganga mkuu waliweza kufika eneo la tukio kwa haraka na kufanya juhudi ili kuokoa maisha yake lakini ilishindikana
Aidha amesema kuwa mipango ya kurudisha mwili Arusha inafanyika na ataendelea kuwajukisha wananchi taratibu zote za msiba huo mkubwa ambao umeukumba mkoa wa Arusha.