******************************************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI la polisi mkoani Pwani ,linamshikilia mtuhumiwa Shaban Athuman 61 mkazi wa Kwamakocho kata ya Mandela Chalinze Pwani ,kwa kosa la kumiliki kiwanda cha kutengeneza silaha na vifaa vya kutengenezea silaha za kienyeji (magobole ).
Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Wankyo Nyigesa ,alisema tarehe 31 majira ya usiku alikamatwa mtuhumiwa akiwa na mtambo wa kufulia vyuma,fataki 48 na risasi 42 za bunduki aina ya gobole.
“Pia alikutwa na chupa 5 ndogo zenye baruti ndani yake ,paketi moja ya unga wa kiberiti ,mitambo mitatu ya silaha ambayo ipo tayari bado kuwekwa mtutu na kitako ,mitambo ya kutobolea vifaa vya miti vinavyofungwa katika silaha aina ya gobole na kopo moja lenye unga wa tindikali ambao unatumika kuunganisha vyuma .”
Aidha Wankyo alieleza,alimatwa pia mtuhumiwa jina limehifadhiwa akimiliki bunduki 3 shortgun 2,na gobole moja ,risasi 13 za shortgun ,maganda 3 ya risasi ,golori 60,misumeno 2 ya kukatia mbao na chuma na kipande cha mtutu wa bunduki .
“Amekutwa na mitambo ya kutengeneza bunduki mbili,plaizi moja ,alieleza Wankyo.
Wankyo alibainisha kuwa,juhudi za kuwatafuta watuhumiwa katika tukio hilo zinaendelea .