************************************************
Kikosi cha Timu ya KMC FC kimeanzakufanya maandalizi kuelekea katika mchezo wake dhidi ya Namungo utakaopigwa siku ya Alhamisi Februali nne mwaka huu katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam saa 10.00 jioni.
Mchezo huo ni kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ya kuanza kuchezwa kwa mechi zilizoahirishwa (Viporo) ambapo KMC FC ni miongoni mwa Timu ambazo mchezo wake dhidi ya Namungo uliahirishwa.
Aidha hadi sasa maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vizuri chini ya Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo na kwamba mpango mkakati ni kuhakikisha kuwa KMC FC inafanya maandalizi ya kutosha na hivyo kuondoka na alama tatu muhimu dhidi ya wapinzani Namungo FC.