Home Mchanganyiko DAS BAGAMOYO AKEMEA VIKALI TABIA YA BAADHI YA WATUMISHI WA AFYA KUIBA...

DAS BAGAMOYO AKEMEA VIKALI TABIA YA BAADHI YA WATUMISHI WA AFYA KUIBA MADAWA

0

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni wa kushoto akizungumza na baadhi ya watumishi hawapo pichani.

…………………………………………………………………………………..

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

SERIKALI wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani imekemea vikali tabia ya  baadhi ya watumishi  wa afya kuamua kukiuka viapo vya kazi zao kwa kujihusisha na vitendo vya wizi wa madawa na kutoa lugha chafu kwa wagonjwa hali  ambayo ni  kinyume  kabisa na maadili ya utekelezaji wa majukumu yao na badala yake wanapaswa wafanya kazi kwa welendi  ili kuepukana na malalamiko ambayo yanatolewa na wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutembelea katika kituo cha afya Kerege kwa ajili ya kuweza kujionea huduma mbali mbali zinazotolewa  na watumishi hao wa afya pamoja na kusikiliza changamoto zilizopo kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.

“Nimeweza kutembelea katika kituo hiki cha afya Kerege ili niweze kuzungumza na watumishi mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuweza kujionea shughuli mbali mbali ambazo zinafanyika ili kuweza kuona namna ya kuweza kuboresha sekta ya afya ili wannachi waweze kupata fursa ya kupata matibabu yanayostahili nah ii itapunguza kwa kiwango kikubwa malalamiko ya wananchi,”alisema Mgeni.

Aidha Mgeni aliongeza kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba inaendelea kuboresha huduma ya afya kwa wananchi na kuwaondolea changamoto mbali mbali zinazowakabili kwa kuweka mipang madhubuti ya kuongeza wataalamu zaidi wa afya ikiwemo kujenga zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali lengo ikiwa ni kuboresha zaidi huduma ya matibabu kwa wananchi.

Pia Katibu huyo alisema kuwa ameakua kufanya ziara zake za kikazi katika maeneo mbali mbali ya zahanati, vituo vya afya pamoja na Hospitali katika Wilaya hiyo ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuibua changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili wauguzi, madaktari pamoja na  watumishi  wa afya ili kuona ni namna gani anaweza kuzisikiliza na kuzifanyia kazi.

Katibu Tawala huyo alisema kwamba inasikitisha sana kuona Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Magufuli kutoa fedha nyingi kwa ajili kuboresha huduma katika sekta ya afaya lakini bado kunakuwepo na baadhi ya wananchi kutoa malalamiko juu ya upatikanaji wa huduma ya afya.

Kadhalika alibaisha kuwa malalamiko mengi ambayo yanatolewa na  baadhi ya wananchi ni kuwepo kwa changamoto ya kucheleweshewa huduma ya matibabu kutokana na baadhi ya watumishi kuomba rushwa na wengine kuwa na lugha ambayo sio nzuri na kutoa huduma kwa upendeleo hali hiyo amabyo inapelekea kuibuka kwa malalamiko hayo.

Katika hatua nyingine amesikitishwa na tazizo la wizi wa madawa katika vituo hivyo vya afya ambapo amedai kumekuwa na baadhi ya watumishi hao kuamua kuiba madawa na kwenda kuyauza katika maduka yao binafsi kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi na kupeleeka ukosefu wa madawa kwa wananchi hao.