………………………………………………………………………
CHUO cha Furahika Education College kinachotoa mafunzo ya elimu ya ufundi bila malipo, kinategemea kufanya mahafali yake ya kwanza Februari 19 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho David Msuya amesema kuwa katika mahafali hiyo itakayoanza kuanzia saa sita hadi kumi na mbili mbili njioni wahitimu 18 wakiwemo wanaume wawili watatunukiwa vyeti na cherehani kwa wahitimu wa fani za ufundi ambazo tayari wameshakabidhiwa.
“Tunawaaomba wananchi na wadau wajitokeze kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kuhakikisha elimu inatolewa bure hasa kumwendeleza mtoto wa kike katika elimu.” Amesema Msuya.
Amesema kuwa kuelekea mahafali hiyo chuo bado kinaendelea kupambana katika kuhakikisha elimu inawafikia vijana wengi zaidi.
“Kuna baadhi ya vijana wa kike wakishajisajili hawahudhurii masomo wengine wanapelekwa kwenye unyago kujiandaa na ndoa…..hivyo lazima wazazi watoe ushirikiano ili kuokoa maisha ya watoto na changamoto za ujauzito usiotarajiwa kwa kuwaleta chuoni kupata ujuzi.” Amesema Msuya.
Aidha amesema wamekuwa wakigharamia masuala mbalimbali katika kuhakikisha watoto hao wanasoma katika mazingira rafiki na kuweza kutimiza malengo yao.
Aidha amesema kuwa, wamekuwa wakitoa elimu ya ufundi yenye malengo ya kumwongezea maarifa watoto kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na Pwani.
Kuhusiana na miradi ya kilimo inayosimamiwa na Taasisi hiyo ya Furahika Msuya amesema kuwa wapo kwenye majaribio ya kilimo cha mbogamboga huku kilimo cha parachichi kikiendelea vyema kuwa wakulima wa Kisarawe na Mkuranga.