Kuelekea katika kilele cha wiki ya sheria kitaifa ambayo kwa mara ya kwanza itafanyika Jijini Dodoma watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Dodoma leo wameshiriki katika mazoezi na mashindano mbalimbali ikiwa ni kuimarisha afya zao.
Akihitimisha tamasha hilo mwenyekiti wa tamasha hakimu mkazi wa Mahakama ya hakimu mkazi Dodoma Denis Mpelembwa amesema wameamua kufanya kitu cha tofauti Kuelekea katika kilele cha wiki ya sheria kwa kukufanyika kwa mahakama zote na kushiriki katika michezo mbalimbali.
“Ikiwa tunasherekea kufikisha miaka mia moja (100) na kufanyika kwa maadhimisho hayo kwa Mara ya kwanza Mkoani hapa tumeona tufanye kitu cha tofauti kidogo watumishi wote tumekutana hapa na kushiriki katika mazoezi na mashindano kwa pamoja” amesema Mpelembwa.
Ametaja baadhi ya michezo iliyofanyika katika tamasha hilo kuwa ni walianza kwa Jogging, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mazoezi ya viungo, Rede na mashindano ya kula na kunywa.
Amesema wameamua kufanya mazoezi kwa pamoja ikiwa ni kuimarisha afya za watumishi na kuamusha ali ya wafanyakazi pamoja na kufahamiana kwa watumishi hao kwa sababu wanatoka katika mahakama za ngazi tofauti tofauti kwa Mahakama Dodoma.
Ameongeza kuwa” tamasha kama hilo ni endelevu ili kuamsha ali kwa watumishi kupitia matamasha kama haya, niombe na taasisi nyingine ziige mfano huu ili kuweza kujenga afya za watumishi wao” amesema.
Nao baadhi ya washiriki wa tamasha hilo wamesema wamefurahi kushiriki tamasha hilo na kuwa wamemepata wasaa wa kukutana na watumishi wenzao wa ofisi nyingine katika kubadilishana uzoefu na kufahamiana.
“Tunaomba tamasha hili liwe endelevu kwa sababu tangu nimefika hapa asubuhi kwa mazoezi na mashindano niliyoshiriki nimejisikia vizuri kwakweli nimefurahi sana” amesema Winnie.