Msanii Rich Lumambo wa muzuki wa asili Msanii wa muziki wa asili Grece Matata.
***************************************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Wasanii wa muziki wa asili(Afro tradition) wameoiomba serikali kuweka usawa kati ya muziki wa asili na muziki wa kizazi kipya(Bongo flavor) unaonekana kupewa kipaumbele zaidi.
Ombi hilo limetolewa na msanii wa nyimbo hizo Rich Lumambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika tamasha la Kan lilianza Januari 28 katika chuo cha maendeleo na uhusiano wa kimataifa(MS-TCDC) kilichopo mkoani Arusha.
Rich Lumambo alisema kuwa wasanii wa nyimbo za asili wanaongelea vitu vinavyokwenda kwenye jamii moja kwa moja hivyo serikali iwape nguvu itayowasaidia kusonga mbele na kufikia usawa wa muziki wa kizazi kipya.
“Muziki wa asili ni muziki wa kuelimisha na unaweza kuwafanya wageni na nchi zingine kuiona Tanzania halisi na umekuwa ajira kwa vijana lakini kwa bahati mbaya tunaenda kama yatima” Alisema Rich Lumambo.
Alifafanua kuwa japo wanapeperusha bendera ya Tanzania wanapopata kazi chache za nje ya nchi lakini wanaenda wao kama wao kwani serikali haiwekezi nguvu kubwa kwao kwani kwa bingo flavor.
Alisema kupitia tamasha la kan wameona limehusisha wasanii mbalimbali na wameweza kupata mafunzo ya kujihusisha na maendeleo ya bara la Afrika ambalo wanaamini wasiweza kupata mahali pengine popote.
Kwa upande wake msanii Grece Matata ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za asili alisema kuwa wasanii wananafasi ya kufungua na kuonyesha fursa zilizopo afrika kwa kutumia sanaa yao.
“Kama wasanii tuna nafasi kubwa ya kusukuma maendeleo ya Afrika na kutangaza utanzania wetu kwa kuendelea kuenzi na kuridhi asili yetu hasa kwa kupitia sanaa ya muziki wa asili ambao tunaufanya sisi,” Alisema Grece Matata.
Alifafanua kuwa muziki ni kitu pekee ambacho hata mtu asipoelewa atapata hisia na hasa kwenye muziki wa asili hivyo watanzania wapende muziki huo na pia waukuze.
Kwa upande wake Khalila Mbowe mkurugenzi wa tamasha la Kan alisema kuwa pamoja na wasanii hao pia G nako, Nikki wa pili Nazizi, Tarajazz Richie, Worriors from the East na Dj Skadi wanatarajiwa kutumbwiza katika hilo kwa lengo la kushiriki katika maendeleo ya bara la Afrika.
“Lengo lao ni kujimuisha bara zima la Afrika kwa kila mmoja kushiriki katika mijadala itayoendeshwa katika mitandao ya kijamii na kuona ni jinsi gani wanaweza kukuza maendeleo ya bara la Afrika hasa kwa kuangalia agenda ya 2063 ya umoja wa mataifa.